MWAKILISHI JAB ASHIRIKI KIKAO KAZI ,UKOKOTOAJI MCHANGO SEKTA YA SANAA



Mwakilishi wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Mawazo Kibamba, akishiriki pamoja na wadau wengine katika kikao kazi cha wataalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhusu ukokotoaji wa mchango wa sekta ya sanaa na burudani katika Pato la Taifa, kilichofanyika Februari 04, 2026 jijini Dodoma.

Akifungua kikao kazi hicho Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Tathmini na Ufuatiliaji Bw. Benard Lubogo amesema kuwa, mafunzo hayo yana lengo la kuwajengea uwezo watalaamu hao namna ya kujua sekta hizo zina mchango gani katika pato la Taifa.

Kwa upande wake Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Pastory Ulimali amesema kuwa Sanaa na burudani ni sekta ambazo zimeajiri watu wengi hivyo Pato la nchi huongezeka kwa idadi ya walipakodi.

#ithibatikidijitali, #Habari #SanaaNaBurudani #PatoLaTaifa #UfuatiliajiNaTathmini JAB WizaraYaHabari Dodoma

Post a Comment

0 Comments