Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Pwani Dkt. David Mramba.
Na Mwandishi Wetu, Kibaha
Katibu wa Siasa ,Uenezi na Mafunzo Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Dkt. David Mramba amesema kuwa hotuba ya Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa tarehe 2 Desemba 2025, alipozungumza na wazee wa Jiji la Dar es Salaam imegusa masuala muhimu yanayohusu Taifa na kutoa dira , matumaini na mwelekeo mpya kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi.
Mwenezi huyo wa CCM Mkoa wa Pwani Dkt.Mramba amesema hayo leo tarehe 5 Desemba 2025 katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika ofisini kwake Makao Makuu ya CCM wa. Pwani.
" Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani kinaunga mkono kwa kauli moja kama ifuatavyo;kuimarisha amani ya Muungano, tunaunga mkono msisitizo wa Mhe. Rais juu ya kulinda amani, utulivu na mshikamano wa Taifa letu kwani amani ndiyo msingi wa maendeleo na hotuba yake imeonesha dhamira ya dhati ya kuendeleza maridhiano,umoja na kudumisha muungano wetu.
Mramba amesema kuwa katika kuchochea uchumi na fursa za maendeleo Chama Cha MÃ pinduzi Mkoa wa Pwani wanapongeza kwa moyo wote maelekezo ya Mhe. Rais kuhusu kuendeleza mageuzi ya kiuchumi ,kukuza utekelezaji, kuimarisha miundombinu na kutengeneza ajira kwa wanawake.
"Katika hotuba ya Mhe.Rais ameweka wazi kuwa Serikali inaendelea kujenga mazingira rafiki ya biashara na kuhakikisha matunda ya uchumi yanawafikia wananchi wake" amesema Dkt. Mramba.
Aidha Dkt. Mramba amesema kuwa Mhe.Rais amesema kuwa atahakikisha anasimamia utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa pia kwamba CCM Mkoa wa Pwani wanaunga mkono kauli ya Mh.Rais ya kuendeleza vita dhidi ya rushwa ,ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka kauli yake imedhihirisha kuwa Tanzania inaongozwa kwa misingi ya haki uwajibikaji na uwazi.
" Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani tunapongeza dhamira njema ya Serikali katika maeneo yafuatayo:
kuimarisha sekta ya afya, kuboresha elimu,kutoa wigo mpana wa upatikanaji wa maji safi, kuhakikisha huduma bora za kijamii kwa wazee,vijana na makundi zinapatikana kwa wakati ,katika kipengele pia ikumbukwe kuwa hotuba ya Mhe.Rais Inaonesha Uongozi shirikishi unaoweka mbele utu na ustawi wa Watanzania" amesisitiza Dkt. Mramba.
Kuhusu ushirikiano wa ushirikishwaji wa wazee amesema ,"CCM Mkoa wa Pwani tunaunga mkono kwa dhati utayari wa Mhe. Rais kusikiliza ushauri wa wazee ,kuthamini mchango wao na kutambua kama nguzo muhimu ya hekima na utulivu wa taifa letu".
Dkt. Mramba amehitimisha kwa kusemakuwa CCM Mkoa wa Pwani wanaunga mkono hotuba ya Mhe. Rais Samia kwa sababu kuu nne ikiwa ni pamoja na kuweka mwelekeo sahihi wa taifa ,inajenga
matumaini kwa watanzania ,inasisisitiza mshikamano na inaweka msingi wa maendeleo endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
" Sambamba na na hayo yote ,Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa wa Pwani tunampongeza Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake mahiri , wenye hekima na wa kijasiri kwa kuonesha uzalendo wa kweli katika kulipigania Taifa.
CCM Mkoa wa Pwani kwa umoja wetu, tunaahidi, kushirikiana na serikali katika kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa kwa manufaa na maslahi ya Taifa letu.Tunamuombea kwa Mwenyeezi Mungu Mhe.Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu afya njema na maisha marefu katika majukumu yake ya kulitumikia Taifa.

0 Comments