WAZIRI KIKWETE AZINDUA JENGO JIPYA TAKUKURU CHALINZE

 

Waziri  wa Nchi  Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi  wa Usimamizi na Utawala Bora (Mb) amewapongeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU kwa kuokoa fedha kiasi cha Bil.60  zilizookolewa kwa kupitia usimamizi wa  miradi mbalimbali. 

Mhe Kikwete ametoa pongezi    tarehe 24 Januari  2026  wakati akizundua  jengo jipya la Ofisi  za TAKUKURU Chalinze Mkoa wa Pwani.

Amewasisitiza TAKUKURU  kutunza Jengo  hilo pamoja na vifaa na samani zilizomo.

Katika hatua ingine Kikwete ametoa pongezi  kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU nchini Crispin Chalamila  kwamba wameonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kutangaza kiasi cha fedha zilizobaki kwenye ujenzi wa Jengo  hilo.

"Kwanza Mkurugenzi wa TAKUKURU acha nikupe maua yako kwa kutangaza hadharani kiasi  cha fedha zilizobaki katika ujenzi  Mil.8 ambazo zitatumika  kwenye miradi mingine huu ni uadilifu wa gali ya juu na umethibitisha kwamba ninyi ni wazalendo  na ukawe mfano  kwenye Taasisi zingine za serikali  nchini  ambapo Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anapitisha fedha  mbalimbali  za miradi pale fedha zinapobaki basi zitangazwe zitafanya shughuli zingine" amesema Waziri Kikwete.

"Namshkuru Rais  Dkt .Samia Suluhu Hassan  kwa  kusimamia utawala bora nchini hivyo na sisi tunao wajibu wa kuipiga vita rushwa  kwa sababu ni adui wa maendeleo  yetu ,natumia jukwaa hili kukuoa maua yako kwa kazi nzuri mliyoifanya kwa taifa  na kuandika historia itakayo dumu kwa taasisi hii muhimu" amesema Mhe.Kikwete.

Mkurugenzi wa TAKUKURU  Crispin Chalamila  amesema  kuwa hadi sasa TAKUKURU wanamiliki majengo 79 na wanachangamoto ya upungufu wa majengo 66.

"Tunaahidi kulitunza jengo hili pamoja na vifaa vyake pia tunawasisitiza wananchi wakaribie kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na vitendo vya  rushwa" amesema Chalamila. 

"Kwa sasa tumekaa eneo lenye utulivu wananchi msiwe waoga  kuleta taarifa  pia tunazo njia nyingi za mawasiliano kuweni huru kuja kutoa taarifa"  amesisitiza Chalamila. 

 Mkurugenzi wa TAKUKURU Chalamila  amesema kuwa bajeti  ya ujenzi wa jengo hilo ilikuwa  Mil.400,006 lakini  hadi jengo linakamika imetumika Mi.400,006.

Chenji mliyoibakisha ni alama kubwa  ya uzalendo na kuonesha kukiishikiapo cha  utii kwamba hata kama ingebaki Shilingi kumi ungeweka wazi  inaonesha kwamba  wewe Chalamila ni Askari namba moja wa kupambana na adui rushwa.

Wakati huohuo amesisitiza  suala la wazawa kupewa kazi katika eneo husika kwani jamii inafaidika katika mzunguko wa fedha amesema hayo kufuatia  Mhandisi Hassan Matula wa Chalinze kuwa ndiye aliyesimamia ujenzi ,kwamba kwakuwa anaishi Chalinze basi kwa kupitia yeye wanachalinze wamefurahia matunda ya kazi hiyo kwa pamoja.

Aidha amesema kuwa taarifa matangazo ya miradi mbalimbali ya  kazi zitangazwe kwa uwazi  kwenye ubao wa matangazo kukwepa  malalamiko na bila kificho.

Pia amewapongeza TAKUKURU  kwa kuanzisha Klabu  132 za wapinga rushwa katika Shule za Msingi na Sekondari  nchini haya ni matunda  mazuri hivyo  yaendelezeni na kurithisha kizazi  cha vijana chuki dhidi ya  rushwa .

"Kizazi kijacho cha Watanzania  kinaonesha  dhahiri  kinachukizwa na vitendo vya rushwa ,fikirieni njia bora za kutokomeza rushwa kama viongozi na sisi watanzania  tuikatae  rushwa kwa vitendo.

Ufunguzi  huo pia umehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge  amesema anawapongeza  TAKUKURU kwa kufanya kazi kwa kuzingatia  uwazi na uwajibikaji  na kwamba  wamejitahidi kuzuia mazingira ya rushwa kwa sababu rushwa inakwamisha  wawekezaji lakini kutokana na jinsi rushwa inavyodhibitiwa ndani ya Mkoa wa Pwani  wawekezaji wamekuwa wakiongezeka siku baada ya siku kuja kuwekeza.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Viongozi  mbalimbali  Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Domina Mkama viongozi wakuu kutoka Idara mbalimbali za TAKUKURU viongozi  wa dini na wananchi.

M


Post a Comment

0 Comments