WAKILI KIPANGULA AMESISITIZA UMUHIMU NA MAJUKUMU YA JAB

 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, akitoa wasilisho kwa wanafunzi wa Mwaka wa Pili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma, kuhusu majukumu na umuhimu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari tarehe 30 Januari, 2026 Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. 

Katika wasilisho hilo, ameeleza majukumu na umuhimu wa JAB, akisisitiza wajibu wa wanafunzi na waandishi chipukizi kusoma, kuielewa na kuzingatia Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229.ya Waandishi wa Habari (JAB), Wakili Patrick Kipangula, akitoa wasilisho kwa wanafunzi wa Mwaka wa Pili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma, kuhusu majukumu na umuhimu wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari tarehe 30 Januari, 2026 Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. 

Katika wasilisho hilo, ameeleza majukumu na umuhimu wa JAB, akisisitiza wajibu wa wanafunzi na waandishi chipukizi kusoma, kuielewa na kuzingatia Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229.

Aidha, Wakili Kipangula amesisitiza umuhimu wa wanafunzi kuwa na ithibati na vitambulisho vya uandishi wa habari wakati wote wanapokuwa kwenye mafunzo kwa vitendo (Field), ili kuwa na uhalali wa kisheria katika utekelezaji wa majukumu yao ya kihabari.

Post a Comment

0 Comments