London, Uingereza –
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mheshimiwa Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mb.), amewasili jijini London kuanza ziara rasmi ya kikazi nchini Uingereza kuanzia tarehe 22 hadi 27 Januari 2026, yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza.
Mara baada ya kuwasili, Mheshimiwa Waziri alifanya kikao cha kazi katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini London, akiwa na mwenyeji wake Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Mbelwa Kairuki, ambapo walijadili masuala ya kuimarisha mahusiano ya kiuchumi, mazingira ya uwekezaji na fursa zilizopo kwa wawekezaji wa Uingereza nchini Tanzania.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mheshimiwa Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mb.), amewasili jijini London kuanza ziara rasmi ya kikazi nchini Uingereza kuanzia tarehe 22 hadi 27 Januari 2026, yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza.
Ziara hii inaashiria mwanzo wa utekelezaji wa mikutano na shughuli mbalimbali ikiwemo kukutana na wawekezaji, taasisi za kifedha, makampuni ya kimataifa na wadau wa maendeleo, kwa lengo la kutangaza fursa za uwekezaji nchini Tanzania na kuendeleza diplomasia ya uchumi.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Prof. Mkumbo anaambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Bw. Gilead Teri.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutumia diplomasia ya uchumi kama nyenzo muhimu ya kuvutia uwekezaji, kukuza uchumi na kuleta maendeleo endelevu kwa manufaa ya wananchi.
📍 London, Uingereza
📅 22–27 Januari 2026
🇹🇿🤝🇬🇧
#TanzaniaUK #DiplomasiaYaUchumi #Uwekezaji
.jpeg)

.jpeg)
0 Comments