Mkuu
wa kitengo cha wajasiliamali wadogowadogo na wakati NMB filbert Mponzi
(katikati)akifurahia kuzinduliwa mkopo wa pikipiki za miguu mitatu
.Wateja wa NMB wataweza kupata pikipiki hizi za miguu mitatu kwa
kupitia matawi ya NMB .Kulia ni Meneja wa Mauzo wa Kampuni ya Fair Deal
Auto Ltd, Anil Dewan na Meneja Masoko wa Kampuni ya Car and
General, Jonathani Masanja.
Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali
Wadogo Wadogo na wa Kati NMB, Filbert Mponzi (kati) Meneja Mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD, Anil
Dewan (Kulia) na Meneja Masoko wa kampuni ya Car and
General, Jonathani Masanja wakifurahia kuzinduliwa mkopo wa
pikipiki za miguu mitatu kwa wateja wa NMB.
Mkuu wa
Kitengo cha wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa kati wa NMB, Filbert
Mponzi (pili kulia) akimpongeza Meneja Mauzo wa kampuni ya Fair Deal
Auto LTD, Anil Dewan baada ya kuzindua mkopo wa pikipiki za miguu mitatu
kwa ajili ya wateja wa NMB, wakishuhudia ni Meneja Masoko wa kampuni ya
Car and General, Jonathani Masanja (pili kushoto) na Meneja wa NMB tawi
la Mbezi, Leonard Ngaya.
Mkuu wa Kitengo cha wajasiriamali
Wadogo Wadogo na wa kati wa NMB, Filbert Mponzi (pili kulia) akimpongeza Meneja Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani
Masanja (pili kushoto) baada ya kuzindua mkopo wa pikipiki za miguu
mitatu kwa ajili ya wateja wa NMB, wakishuhudia ni Meneja Mauzo wa kampuni ya
Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan na Meneja wa NMB tawi la Mbezi, Leonard Ngaya.
DAR ES SALAAM, Tanzania
BENKI ya NMB
kwa kushirikiana na kampuni mbalimbali zinazosambaza pikipiki za miguu mitatu, imeanzisha
mikopo ya pikipiki hizo kwa wateja wake kwa lengo la kuwapatia unafuu wa
kujikimu kimaisha huku wakiendelea na shughuli zao za kila siku.
Mikopo hiyo
yenye masharti nafuu itatolewa kwa mteja yeyote mwenye kukidhi vigezo
vilivyowekwa ikiwa ni uwezo wa kulipia asilimia 30 ya gharama au bei ya pikipiki
kama inavyouzwa na kampuni hizo ambazo ni
Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina
ya Bajaji pamoja na kampuni ya Car and General Ltd inayosambaza
inayosambaza pikipiki ya miguu mitatu aina ya TV’S King.
Akizindua
huduma hiyo katika tawi la Mbezi Beach jana, Meneja Mwandamizi wa wajasiriamali
wadogo na wa kati Filbert Mponzi amesema kuwa, gharama za pikipiki hizo
hutofautiana kulingana na kampuni husika.
Alisema kuwa,
bajaji inayosambazwa na kampuni ya Fair Deal Auto Private Ltd kwa sasa inauzwa
sh. milioni 5.4 huku TV’S King inayosambazwa na kampuni ya Car and General Ltd
ikiuzwa kwa sh. milioni 5.6.
Alisema, mikopo
hiyo hutolewa kwa muda wa miezi 24 ambapo kwa kipindi hicho chote mteja
ataendelea kurejesha makato ya kila mwezi kulingana na makubaliano
yatakayofanyika baina yake na benki.
Aidha,
mikopo hiyo inawekewa bima itakayomletea mkopaji unafuu wa kumalizia deni hasa
pale atakapopata matatizo ya kiafya yatakayomfanya asiwe na uwezo wa kuendelea
na shughuli zake za kila siku au hata kufariki kwani bima hiyo itamalizia deni
na mteja ataendelea kumiliki pikipiki yake.
Aliongeza
kuwa, wateja wa NMB sasa wanaweza kutimiza ndoto zao za kumiliki pikipiki ya
miguu mitatu kwa kutumia mikopo hiyo.
Mikopo hiyo
kwa sasa hutolewa katika matawi tisa tu ya NMB yaliyopo jijini Dar es Salaam
ambazo ni NMB Temeke, NMB Tegeta, NMB Mbezi, NMB Ilala, NMB Airport, NMB
Mlimani City, NMB Magomeni pamoja na NMB Msasani.
NMB haitaishia
hapo kwani itaendelea kufanya mikakati mikubwa ili kuhakikisha huduma hiyo
inawafikia wateja wake walioko katika mikoa mingine hapo baadaye.
0 Comments