Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka
akiwasalimia wakazi wa kata ya Bunju na Wazo mara baada ya kuwasili
katika eneo hilo kwa lengo la kuzungumza nao ili kutafuta suluhisho la
kudumu la mgogoro wa ardhi kati yao na kiwanda cha Saruji cha Twiga
jana jioni.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiongea
katika mkutano wa hadhara na maelfu ya wakazi wa kata ya Wazo na Bunju
waliojitokeza kufuatilia maendeleo ya mgogoro wa ardhi kati yao na
Kiwanda cha Twiga Cement ambapo pamoja na mambo mengine amewahakikishia
wakazi hao kuwa mgogoro huo utapatiwa ufumbuzi wa kudumu na kuwaomba
kutoa ushirikiano kwake.
Diwani
wa eneo la Bunju na Wazo Sharif Exavery Majisafi akiongea na wananchi
kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna Tibaijuka kuzungumza nao.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka akipitia
baadhi ya nakala za ramani zinazoonyesha eneo la Kata ya Bunju na Wazo
pamoja na Kiwanda cha Saruji cha Twiga ambazo ziligawiwa kwa wananchi.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt. Silasi Mayunga.
Sehemu
ya umati mkubwa wa wakazi wa kata za Bunju na Wazo wakimsikiliza kwa
makini Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna
Tibaijuka.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka (kulia)
akiongea na Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Saruji cha Twiga (Twiga
Cement) Bw.Pascal Lessoinne (kushoto) mara baada ya mkurugenzi huyo
kutoa taarifa fupi ya maendeleo ya kiwanda hicho na hali ya mvutano wa
muda mrefu wa umiliki wa maeneo baina ya wakazi wa kata za Bunju na Wazo
jijini Dar es salaam.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja ambaye jina lake halikuweza
kupatikana mara moja katikati ya wananchi wenzake akiwa amevaa kofia
ngumu ya waendesha pikipiki wakati wa mkutano wa hadhara wa wakazi wa
kata ya Bunju na Wazo na Waziri wa Ardhi Prof. Anna Tibaijuka kujadili
mgogoro wa ardhi kati yao na Kiwanda cha Twiga Cement. Haikujulikana
mara moja lengo la kuvaa kofia hiyo licha ya mkutano huo kutawaliwa na
amani na maelewano makubwa.
0 Comments