Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino
International Agency,waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga, akizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es
Salaam leo wakati wa kutangaza zawadi za Mshindi wa Shindano la Redds Miss
Tanzania 2012. Kulia ni Meneja wa Kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro.
Kampuni ya TBL kupitia kinywaji
chake cha Redds Original ambao ndio Mdhamini mkuu wa shindano la Redds Miss
Tanzania 2012, leo tunatangaza zawadi kwa washiriki wote wanaowania taji la
Redds Miss Tanzania 2012.
Akizungumza na waandishi wa Habari
Jijini Dar Es Salaam jana Mkurugenzi wa
Kampuni ya LINO INTERNATIONAL AGENCY Hashim Lundenga alisema katika fainali za
shindano la Redds Miss Tanzania 2012 zitafanyika tarehe 3 Novemba 2012 katika
ukumbi wa Blue Pearl Hotel, (Ubungo Plaza) jijini Dar es salaam ambapo ni
shindano linaloshirikisha washiriki 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Leo hii tunapenda kuchukua nafasi
hii kuwatangazia rasmi kuwa katika fainali ya Redds Miss Tanzania mwaka zawadi
zitakuwa kama ifuatavyo
1) Mshindi
wa Kwanza atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 8,000,000/- Pamoja na gari
2) Mshindi
wa pili atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 6,200,000/-
3) Mshindi
wa tatu atapata zawadi ya pesa taslmu shs: 4,000,000/-
4) Mshindi
wa nne atapata zawadi ya pesa taslimu shs; 3,000,000/-
5) Mshindi
wa tano atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 2,400,000/-
6) Mshindi
wa sita hadi wa 15 kila mmoja atapata shs: 1,200,000/-
7) Washiriki
wengine wote waliobaki kila mmoja atalipwa shs: 700,000/-
Katika
shindano hilo ambalo ndani yake kuna mashindano mengine madogo [Fast Tract]
tayari washiriki 3 wameshajipatia tiketi ya kuingia katika
[Top 15 Finalist]
Washiriki
hao ni Lucy Stephano – Miss Photogenic
Magdalena
Roy – Top Model
Mary
Chizi – Top Sport Woman
Shindano
dogo lingine limepangwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 26 Oktoba 2012 la
kumtafuta mrembo wenye Kipaji. Miss Talent.
Na
tarehe 28 Oktoba 2012 atapatikana Miss Personality.
Nae
Meneja wa kinywaji cha Redds Original Bi Victoria Kimaro amesema huu ni wakati
sahihi wa kumpata mshindi biomba mwenye vigezo sahihi hivyo kuwataka wapenzi
wote wa tasnia ya urembo na wapenda maendeleo kote nchini kujianda kupata
tiketi za kushudia fainali hiyo mapema ili kuweza kupata fursa ya kupata
burudani mbalimbali.Kwa kweli shindano la mwaka huu tunatarajia kuwa litafana
sana hasa kwa kuzingatia kuwa maandalizi yote yameshakamilika kwa kiwango
kikubwa na sisi kama wadhamini wakuu tunahakikisha kuwa mwaka huu kila
atakaefika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza atakuwa na jambo la kusimulia kwa
sababu ni shindano la kipekee.
Shindano hili la Redds Miss Tanzania 2012 linadhaminiwa na
.Redds
Original,Star
TV,Giraffe
Hotel.
0 Comments