Mafunzo hayo ambayo yanayotolewa na wataalam mbalimbali yamejikita kwenye mada zinazohusu Haki jinai, Afya ya akili, Itifaki, uwekezaji, uongozi na nidhamu kwa watumishi yanafanyika kuanzia tarehe 31 Agosti hadi 4 Septemba 2026 Jijini Mwanza.
Akifungua mafunzo hayo mshauri wa Jeshi la Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro Kanali Fikiri Machibya amewataka askari hao kufanya kazi kwa kuzingatia nidhamu na utu kwa kila raia.
Kanali Machibya amesema askari wa uhifadhi wana jukumu la kulinda rasilimali za nchi kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni.




0 Comments