WASANII NA WAANDISHI WALIPOKUTANA USIKU WA TAREHE 2 MJINI MBEYA



 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wageni waalikwa kwenye sherehe za Usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari zilizofanyika usiku wa tarehe 2 Februari kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Mbeya.
 Mbunge wa Mbinga Magharibi Kapteni John Komba akizungumza na waandishi wa habari na wasanii wa muziki na sanaa za filamu Tanzania kwenye siku ya Usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Mbeya, katika usiku huo Komba alisisitiza wasanii kuangalia maisha yao ya mbele na sio sasa kwani wasipojiandaa wataaibika hapa ulimwenguni pia alisisitiza juu ya maslahi ya wasanii kuongezwa kutokana na kazi kubwa wanazofanya na thamani ya kazi wayofanya.
 Wasanii wakimpongeza Kapteni John Komba kwa wosia mzuri aliotoa juu yao .
 Msanii Maarufu nchini Hafsa Kizinja akitumbuiza siku ya usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari,Februari 2 mjini Mbeya ,siku ambayo CCM ilisheherekea miaka 37 ya kuzaliwa kwake na kitaifa sherehe hizo zilifanyika mjini hapo.
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali wakijumuika kumshangilia Mwenyekiti wao wa Kikosi cha Ziara mkongwe Richard Mwaikenda akijimwaga wakati wa sherehe za Usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari zilizofanyika tarehe 2 Februari siku ambayo CCM ilisheherekea kutimiza miaka 37 ya kuzaliwa kwake na sherehe kufanyika kitaifa mkoani Mbeya.
 Wasanii wa tasnia ya Filamu wakiwa wamepozi kwenye sherehe za usiku wa Wasanii na Waandishi
 Msanii wa Siku Nyingi nchini Dokii akisalimiana na  Mwigulu Lameck Nchemba Naibu Waziri Wizara ya Fedha (Sera) wakati wa sherehe za usiku wa Wasanii na waandishi wa Habari.
 Baadhi ya waandishi kutoka Jjiji la Mbeya wakipata vinywaji na maongezi kidogo wakati wa sherehe fupi za kukutana pamoja na waandishi na wasanii wa muziki na filamu zilizofanyika tarehe 2 Februari mjini Mbeya.
 Waandishi wa Umoja wa Waandishi wa Habari mkoani Mbeya wakizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa sherehe fupi za kupongezana kwa kazi nzuri wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM lakini pia usiku huo ulipewa jina la Usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari.
 Wasanii wakongwe wa tasnia ya filamu Tanzania nao walikuwepo kutoka kushoto ni Baba Haji, JB na Rich.
 Kila mtu maarufu alikuwepo kwenye tasnia ya sanaa za maigizo na filamu.
 Malkia wa Taarab nchini Hadija Kopa akitoa vionjo vya nyimbo yake mpya ambacho kinasema hata Obama anamjua.
Katibu wa NEC Itikadi na Unenezi wa CCM Nape Nnauye akiimba sambamba na band ya TOT wakati wa usiku uliopewa jina la usiku wa Wasanii na Waandishi wa habari.

Post a Comment

0 Comments