Mrembo atakaewakilisha Tanzania
katika mashindano ya mwaka huu ya Miss East Africa
ni
Jocelyne Diana Maro (22).
Jocelyne Diana Maro (22).
Mrembo huyo alipatikana kufuatia mchakato ulioendeshwa na
kamati maalum ya kuratibu zoezi hilo kwa zaidi
ya miezi mitatu iliyopita na kuwashinda warembo wengine 148 waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Tanzania
katika mashindano ya Miss East Africa 2012
Jocelyne amehitimu shahada ya Business Economics mwezi wa
saba mwaka huu katika chuo kikuu cha Keele
University, Nchini
Uingereza
Maandalizi ya
mashindano hayo yanaendelea vizuri na yapo kwenye hatua za mwisho ikiwa ni
pamoja na kukamilisha taratibu zote za BASATA ili kufanikisha mashindano hayo yatakayofanyika
tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu tayari yameanza
kuvuta hisia za watu wengi barani Africa kufuatia kiwango cha juu cha warembo
wanaowania taji hilo.
Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.
Mashindano ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano
na kutangaza utamaduni wa Afrika Mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania
kama Nchi wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika
Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na
kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,
Rena Callist,
Executive Producer,
0 Comments