KATIKA tukio la kushangaza hivi karibuni mchumba wa msanii wa kizazi kipya, Jaffari Mshamu ‘Jaffarai’, ambaye ni mgombe ubunge kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Kinondoni, Shy-Rose Bhanji, ametoa mpya kwa kusema kuwa bado hajaolewa na wala hana mchumba.Kauli hiyo aliitoa na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari wakati akijinadi na kuzusha maswali mengi kama tayari mwanamama huyo amemmwaga mwimbaji Jaffarai, ambaye amekuwa akimuimba mara kadhaa katika nyimbo zake.
Moja ya nyimbo ambazo msanii huyo amemuimba karibu wimbo wote ni ‘Mi naye’.
0 Comments