Kutoka kushoto Katibu Gospel House of Tanzania Charles Gao, Mratibu wa tamasha Harris Kapiga na Mkurugenzi wa Imuka Singers (COSAD TZA) Smart Baitan
Imuka Singers” ni mkusanyiko wa vikundi mbalimbali vya kwaya na vikundi vya sanaa vilivyopo mkoani Kagera. Mnamo May 25 2009, chini ya uongozi wa ndugu Smart Baitani, zaidi ya vikundi 27 vilichagua wawakilishi na kuunda kikundi kimoja chenye wasanii waliobobea katika sanaa na utunzi kwa ajili kuunganisha nguvu ya pamoja ili kutumia muziki na sanaa kama kioo cha jamii ya Mtanzania na kutatua matatizo ya kiuchumi katika jamii inayowazunguka.
- CHIMBUKO NA MALENGO YA IMUKA SINGERS:
i) CHIMBUKO: Chimbuko la Imuka Singers ni UPENDO na NIA ya kutaka kuona jamii nzima ya Tanzania tunaishi maisha ya mafanikio kwa kutumia vipaji vyetu tulivyopewa na Mungu na raslimali tulizonazo kuleta maendeleo endelevu.
ii) MALENGO: Malengo ya Imuka yamegawanyika katika sehemu kuu mbili:
a. Kuhamasisha jamii ya Kitanzania na Afrika kwa ujumla juu ya shughuli za maendeleo ya kiuchumi na kiutamaduni na pia kuwa mstali wa mbele katika kulinda maadili ya jamii na utamaduni wa Mtanzania. (Social Enterprise Mission of Imuka)
b. Kutangaza shughuli za maendeleo na maisha ya jamii yetu nje ya nchi kwa kushirikiana na wadau wake Marekani na duniani kote. (Cultural Outreach Mission of Imuka).
2. UPEO NA UPANA WA SHUGHULI ZA IMUKA (SCOPE AND STRATEGIC VISION):
i) Tanzania na East Africa kwa Ujumla:
a) Kupitia shirika Mama, COSAD Center (Community Solutions for Africa’s Development) kushirikiana na vikundi mbali mbali vya jamii ikiwemo makanisa kunadaa matamasha kwa ajili ya kuinua vipaji na kutoa elimu na maadili ya utamaduni wa Mtanzania na Afrika kwa Ujumla.
b) Kupitia shirika Mama, COSAD Center (Community Solutions for Africa’s Development) kushauri, kuboresha, kukusanya shughuli za kiuchumi hasa zile za kitamaduni na kazi za mikono kwa ajili ya kuzitafutia masoko nje ya nchi.
c) Mpaka sasa Imuka inashirikiana na waimbaji, na wanasanaa 30 kutoka vikundi zaidi ya 20 vilivyomo mkoani Kagera. Mipango endelevu ni kushiriana na vikundi toka pande zote za Tanzania vilivyo na nia siyo ya kuimba kwa ajili ya kutumbuiza tu (beyond entertainment) lakini pia kutumia vipaji kwa ajili ya kuleta maendeleo ya jamii nzima ya Mtanzania. Mazungumzo tayari yameisha anza kati ya hasasi mbali mbali ikiwemo, Tanzania Gospel House of Talent kwa ajili ya kuanza kuandaa matamasha makubwa ya pamoja ili kupitia matamasha haya kuchagua washiriki wa ziara (concerts) za kila mwaka za Marekani na Canada ambazo Imuka ilikuwa ikizifanya kwa wanamuziki wa Kagera.
ii) Nchini Marekani na Canada: Katika kuhakikisha Imuka Singers inafanya biashara na shughuli zake kwa dhati ilifungua ofisi zake nchini Marekani katika mji wa Minneapolis, Minnesota.
Mwaka 2011, Imuka Singers ilizuru nchini Marekani na kufanya tamasha 52 zilizofana sana katika majimbo mbalimbali ikiwemo: Minnesota, Illinois-Chicago, California, Michigan na Wisconsin.
Lengo kubwa la ofisi za Imuka Marekani ni:
a) Kundaa matamasha ya kila mwaka katika mashule, vyuo vikuu, makanisani na kumbi mbali mbali. Imuka kila mwaka upeleka Kikundi cha wasanii wa Muziki na sanaa wapatao 20 kufanya concert zaidi ya 50.
b) Kutafuta masoko na kuuza bidhaa za kazi za mikono kutoka Tanzania na Afrika ya Mashariki kwa ujumla. Hii ni pamoja na kutafuta wawekezaji (partners) wa kushirikiana na wazalishaji wa bidhaa hizi.
- MAWASILIANO NA USHIRIKI (CONTACTS AND PARTNERSHIPS INQUIRIES)
Unaweza kuwasliana nasi kujua ni jinsi gani tunaweza kushirikiana kujenga jamii na taifa letu kupitia anwani zifatazo:
USA: Imuka Singers, Inc. | COSAD Inc.
Attn: Smart Baitani, President and Artistic Director,
Minneapolis, Minnesota,| Bukoba, Tanzania
Tel: 612 227 0065 (USA) + 255 786 024 210 (Tanzania)
Email: smart@cosad.org | Website: www.imukasingers.org | www.cosad.org
Dar es Salaam, Tanzania: Gospel House of Talent-Tanzania
Harris Kapiga | Cloud FM | +255 715 48.47.37
Charles Gao | Tel: 255 712 703986
Bukoba: The COSAD Center | Imuka Cultural Creativity Center
Cassian Rweyendera | COSAD Center | +255 757 523929
Lydia Lutemba | Imuka Cultural Dance Ensemble | +255 754 201148
0 Comments