ZAMBIA WASHINDI WA FINAL ZA AFRICA CUP OF NATIONS.


Wazambia walijitokeza mitaani nchini humo kwa wingi mapema Jumatatu mara tu baada ya timu yao ya taifa kushinda kombe la mataifa Afrika baada ya kuifunga Ivory Coast 8-7 kwa penalti katika mechi ya fainali mjini Libreville, Gabon.


Ulikuwa ushindi uliokuwa na maana ya pekee kwa Zambia mjini Libreville. Wiki iliyopita wachezaji wa timu ya Zambia waliweka mashada ya maua katika eneo karibu na mahali ambapo ndege ya kijeshi ya Zambia iliangukia baharini mwaka 1993, na kuuwa wachezaji wote wa timu ya taifa na maafisa wa timu hiyo, jumla ya watu 25.

Mwaka ule wa 1993 radio ya taifa ilisimamisha matangazo ya kawaida na kutangaza kuanguka kwa ndege hiyo katika lugha nane zinazozungumzwa rasmi Zambia. Mjini Lusaka watu - wanawake kwa wanaume - walilia katika maofisi na mitaani.
Jumatatu, ilikuwa ni sherehe tupu.

Wazambia waliokuwa wamebeba bendera ya taifa hilo walijazana mitaani, wengine wakichungulia kutoka madirishani na kuimba nyimbo zinazoendana na mchezo wa mpira wa miguu,

Kabla ya mechi hiyo ya fainali, Wazambia hawakukubali utabiri wa wengi barani Afrika na nje kuwa Ivory Coast itashinda mechi hiyo, lakini vijana wa Chipolopolo walionyesha kuwa wameingia katika kiwango cha juu barani Afrika kwa kupata ushindi baada ya mechi kumalizika sare.

Rais Michael Sata aliwakilishwa katika mechi hiyo ya fainali na Makamu Rais Guy Scott pamoja na rais wa zamani Kenneth Kaunda na Rupiah Banda, pamoja na ndege mbili za mashabiki wa Zambia ambao waliondoka Lusaka mapema Jumapili asubuhi kuelekea Libreville.
Wazambia washerehekea ushindi wa Kombe la Afrika
Ushindi wa Zambia umekuja katika ardhi ambayo miaka 19 iliyopita ndege iliyobeba timu ya taifa ya nchi hiyo ilianguka na kuuwa wachezaji wote

Post a Comment

0 Comments