YALIYOJIRI KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF)





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI24/05/2011

UCHAGUZI WA VIONGOZI WA VYAMA VYA MPIRA WA MIGUU VYA WILAYA

1. Kamati inawataka wanachama wote wa TFF kwa ngazi zote kukamilisha uteuzi wa wajumbe wa Kamati za Uchaguzi kabla ya tarehe 31 Mei 2011 kama yalivyo maelekezo ya TFF kwa wanachama wake yaliyotolewa mwanzoni mwa mwezi Aprili 2011.

2. Kamati ya Uchaguzi ya TFF inavitaka vyama vya mpira wa miguu vya wilaya ambavyo muda wa ukomo wa madaraka ya uongozi umekwisha/umekwishapita vianze mara moja mchakato wa uchaguzi.

Vyama hivyo vinaagizwa kushirikiana na Kamati za Uchaguzi za vyama vya mpira wa miguu vya Mikoa kuhakikisha kuwa vinafanya uchaguzi kabla ya tarehe 31/07/2011, kwa mujibu wa maagizo yaliyotolewa na TFF mwezi Aprili 2011, na vifanye hivyo kwa kufuata Katiba zinazoendana na Katiba ya mfano ya TFF na kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF.

KAMATI YA UCHAGUZI -TFF

Post a Comment

0 Comments