Ni kijana wa makamo hivi ambaye alionyesha kipaji cha kufreestyle kwa kiwango cha juu kabisa,anaitwa Rota Flavian Komba ndiye aliyeibuka kinara wa msimu wa dhahabu wa unaoendelea na Serengeti Fiesta Freestyle 2011 ndani ya mji wa Morogoro jioni ya leo.Kufuatia ushindi huo Rotas atakwenda jijini Dar kupambana na vinara wengine kutoka mikoa mingine katika mpango mzima wa kutimiza kilele cha msimu wa dhahabu na Serengeti Fiesta 2011 ndani ya jiji la Dar,itakayofanyika hapo baadaye
Pichani kulia ni Rota akishusha mistari yake katika mtindo huru mbele ya hasimu wake Hanstar,katika mtindo ule wa Kubato,wakiwa katika hatua ya mwisho a.k.a fainali,kwamba atakayeshinda ndiye kinara wa msimu wa dhahabu wa unaoendelea na Serengeti Fiesta Freestyle 2011 ndani ya mji wa Morogoro jioni ya leo.
Pichani ni Washiriki Wanne kati ya washiriki 44 walioingia nusu fainali katika suala zima la kumsaka mkali wa msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta Freestyle 2011,kutoka kulia ni Rotas,Slim,Ras Q pamoja na Hanstar.

0 Comments