KAGERA SUGAR WAICHAPA TRANSIT CAMP NYUMBANI 


Timu ya soka ya Kagera Sugar ya Bukoba  jana  wametoka kifua mbele kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Timu ya Transint Camp kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza waliocheza mwishoni mwa wiki  katika Uwanja wao wa Nyumbani Filbert Bayi Mkuza Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mechi hiyo kumalizika Kocha wa Kagera Sugar Juma Kaseja 'Tanzania One' amesema kuwa licha ya ushindi huo kuna maboresho yanahitajika hasa kwa  waamuzi ili wachezeshe mpira kwa kuzingatia maadili na kanuni  za mpira.
"Tunaposema  tunahitaji maboresho ya viwanja siyo kwamba viwanja ni vibaya la hasha, tunahitaji  marefarii watoe maamuzi ya sahihi ni hivyo tu," amesisitiza  Kaseja.
"Mchezo ulikuwa mgumu hasa katika kipindi cha kwanza  hadi tunakwenda mapumziko Transit Camp walikuwa wanaongoza kwa goli moja  na kwamba timu zote zilikuwa zimekamiana kimchezo".
Kaseja amesema wamejipanga katika michezo yake ijayo watajipanga ili wapate  matokeo mazuri zaidi.

Kwa upande wake Kapteni wa Timu ya Transit Camp Issa Dau amekiri kushindwa na kuwapongeza Kagera Sugar, kwa kusema walizidiwa katika kipindi cha pili  ambapo wenzao walizitumia vizuri nafasi na kufanikiwa kuwafunga.

 Naye Kocha wa Timu ya Transit Camp Shadrack Nsajigwa  amekiri kuzidiwa kete na Kagera Sugar  pia amewapongeza wa kunyakua pointi tatu.

"Kagera Sugar  wamefanya vizuri katika kipindi cha pili  mimi na wachezaji wangu tutaanza mazoezi Jumatatu (leo)  huko ndiko tutajua namna ya kutafuta mbinu za kushinda" amesema Nsajigwa.

Post a Comment

0 Comments