Aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu (27) , mkazi wa Sinza Jijini Dar es Salaam leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo ya Kinondoni kwa kosa la kutukana hadharani.
Ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa huyo alimtukana matusi ya nguoni msanii wa kizazi kipya, Raheem Rummy 'Rais wa masharobaro' ambapo ameshitaki kosa lake.
Hata hivyo mshitakiwa huyo alidai mahakamani hapo kuwa aliamua kumtukana mshitakiwa kwa sababu ya dharau zake alizokuwa anamfanyia.''Mheshimiwa Hakimu si kawaida yangu kutukana ovyo ovyo, lakini hasira zimenifanya nifanye hivyo na ndiyo maana nimekubali kosa langu.
Mbele ya Hakimu Mariamu Masamalo, ilidaiwa na Karani Sharifa Dunia kuwa, Aprili 11 mwaka huu 2011, Kinondoni, mshitakiwa alimtukana mlalamikaji huyo na kesi imeahirishwa mpaka Aprili 18 mwaka huu.Hii itakuwa ni mara ya pili kwa mrembo Wema kupandishwa kizimbani katika kipindi cha mwaka mmoja nyuma alipanda kujibu kosa la kumfanyia fujo msanii nyota wa filamu nchini , Steven Kanumba baada ya kuvunja kioo cha gari.
Aidha aliachiwa kwa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili kwa sh. 300,000 kila mmoja.
1 Comments