USAJILI KILI TAIFA CUP 2011 WAKAMILIKA

Kamati ya Mashindano ya TFF ilikutana jana ambapo pamoja na mambo mengineilipitia maombi ya usajili kwa timu zinazoshiriki michuano ya Kombe la Taifa(Kili Taifa Cup 2011) inayoanza Mei 7 mwaka huu katika vituo sita vya Lindi,Mbeya, Morogoro, Moshi, Mwanza na Tabora

Usajili wa wachezaji wote umepitishwa isipokuwa wawili tu. Wachezaji hao ni Nurdin Mussa Mponda aliyeombewa usajili timu ya Mkoa wa Temeke na Kudura HamisMaguta aliyeombewa Kinondoni.

Wachezaji hao waliombewa usajili kinyume na kanuninamba 33 ya michuano ya Kombe la Taifa.

Mponda msimu huu amechezea Villa Squad ya Kinondoni, hivyo hakuwa na sifa yakuchezea timu ya Mkoa wa Temeke wakati Maguta alichezea Moro United ya Mkoa waIlala ingawa aliombewa usajili akioneshwa kuwa ni mchezaji wa Red Coast.

Ukiondoa Ligi Kuu, kanuni inataka wachezaji wa madaraja mengine wachezee mkoaambao timu zao la ligi zimesajiliwa.

SIFA ZA MAKOCHA

Kwa mujibu wa Kanuni ya 42 ya michuano hiyo, makocha wakuu wa timu za mikoawanatakiwa kuwa na cheti cha ngazi pevu (Advance Level) wakati wasaidiziwanatakiwa kuwa na cheti cha ngazi ya kati (Intermediate Level).

Hivyo Kamati imezikumbusha timu zote zinazoshiriki michuano hiyo kutokwendakinyume na sifa hizo kwa vile tayari zina kanuni za mashindano.

LIGI YA TAIFA 2011

Ligi hiyo inayoshirikisha mabingwa wa mikoa imepangwa kuanza Juni 11 mwaka huukatika vituo vya Kigoma, Mbeya, Pwani na Singida ambavyo vilishatangazwa awali.

Usajili utafanyika kuanzia Mei 10 hadi 25 mwaka huu wakati kipindi cha pingamizini kuanzia Mei 26 hadi Juni 3 mwaka huu. Usajili utapitishwa Juni 4 mwaka huu wakati ada ya kushiriki ni sh. 70,000 nakadi ya mchezaji ni sh. 6,000 ambapo timu zinatakiwa kulipa wakati wa kurejeshafomu za usajili.

Mikoa ambayo imewasilisha rasmi TFF mabingwa wao ni Dodoma (Majengo FC), Kigoma(Kasulu United), Kilimanjaro (Lang’ata Bora FC), Morogoro (Tumbaku) na Mwanza(Geita Veterans).

Hivyo, Kamati imeagiza mikoa ambayo haijawasilisha majina ya mabingwa waokufanya hivyo haraka, kwani ikishindwa ligi itaendelea kwa tarehe zilizopangwabila timu zao kuwemo.

Vilevile mikoa ambayo imemaliza ligi zao, lakini bingwahajapatikana kutokana na rufani, zimetakiwa kusikiliza rufani hizo haraka

LIGI KUU YA VODACOM 2010/2011

Kamati imemfungia mechi tatu za ligi hiyo Daktari wa Yanga, Juma Sufiani baadaya kumsukuma mchezaji mmoja wa Azam kwenye mechi kati ya timu hizo iliyochezwaMachi 30 mwaka huu Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Atatumikia adhabu hiyokuanzia msimu ujao wa ligi. Mwamuzi wa mechi hiyo alimtoa kwenye benchi kutokanana kosa hilo.

Suala la mchua misuli wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein kumtukana mwamuzimsaidizi Saada Hussein, na lile la mshambuliaji wa timu hiyo Gaudence Mwaikimbakuwafuata waamuzi vyumbani na kuwatukana baada ya mechi dhidi ya AFC 10 mwaka huu Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba yamepelekwa Kamati ya Nidhamu.

Kwa mujibu wa Kanuni, makosa yote ya kinidhamu yanayotokea nje ya uwanja adhabuzake zinatolewa na Kamati ya Nidhamu ambayo kwa sasa inaongozwa Naibu Kamishnawa Polisi (DCP) mstaafu Alfred Tibaigana.

Boniface Wambura

Ofisa Habari TFF

Post a Comment

0 Comments