BURIANI SHEIKH YAHYA HUSSEIN,KUZIKWA LEO KATIKA MAKABURI YA TAMBAZA DAR ES SALAAM

Pichani ni marehemu Sheikh Yahya Hussein ambaye pia alikuwa Mnajimu Mkuu wa Nyota Afrika Mashariki na kati, aliyefariki jana asubuhi Mei 20 2011, kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa moyo alipofikwa na mauti katika Hospitali ya Mount Ukombozi iliyopo maeneo ya Morocco Kinondoni Jijini Dar es Salaa. Jeneza la marehemu lisasaliwa katika Msikiti wa Tambaza pia atazikwa katika makaburi ya Tambaza Jijini Dar es Salaam.Shughuli za maziko zitaanza Saane asubuhi nyumbani kwake Magomeni Mwembechai.


Wakati huohuo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Sheikh Yahya kufuatia kifo hicho."Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Sheikh Yahya Hussein ambaye katika enzi za uhai wake alijipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi kwa kupitia kipaji chake katika masuala ya unajibu wa nyota naomba kama familia mpokee salamu zangu za pole kwa kuondokewa na kiongozi na tegeo katika familia".Marehemu Sheikh Yahya alizaliwa 1922 Ujiji Kigoma na kuhitimu ipasavyo elimu yake ya Dini katika Madrasa ya Ghazal iliyo Ujiji Kigoma.


Blog ya Bongoweekend imeguswa na msiba huu hivyo naungana na wanafamilia ya Sheikh Yahya katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Baba, babu, mjomba hivyo hatuna budi kumshukuru Allah kwa kila Jambo licha ya kwamba niko nje ya Dar es Salaam naungana nanyi katika kumrehemu marehemu .Innalillah Wainna Ilaih Rajiun.

Post a Comment

0 Comments