UWT KIBAHA MJI YAFANYA KWELI YAADHIMISHA MIAKA 49 YA CCM KWA KUPANDA MITI

 

Jumuiya ya umoja wa wanawake Wilaya ya Kibaha mjini (UWT) katika kusherekea maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi (CCM) kimeamua kuunga juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha mazingira kwa kupanda miti katika Kata ya Mkuza.

Maadhimisho hayo ambayo yamefanyika katika kata ya Mkuza na kuhuduliwa na viongozi mbali mbali wa chama pamoja na jumuiya zake yalikwenda sambamba na kuzungumza na wanancham wa CCM, pamoja na kufanya matendo ya huruma kwa viongozi wa matawi kwa kutoa msaada wa mahitaji mbali mbali pamoja na fedha kwa ajili ya kuweza kujikimu.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonja amesema kwamba wameamua kusherekea maadhimisho ya kuzaliwa kwa chama kwa kupanda miti ikiwa pamoja na kufanya matendo ya huruma kwa baadhi ya viongozi katika tawi la Bungo lililopo katika Kata ya Mkuza .

"Kwa upande wetu sisi kama UWT Wilaya ya Kibaha mjini tupo katika maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa CCM kwa vyo tumeungana na wenzetu kutoka kata mbali mbali kwa ajili ya kufanya ziara ya kuzungumza na wanachama wetu ikiwa sambamba na kuendesha zoezi la upandaji wa miti ikiwa ni moja ya kumuunga mkono Rais wetu wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassa,"alisema Mgonja.

Aidha Mwewnyekiti amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo ikiwa pamoja na kutenga fedha nyingi ambazo zimeweza kwqenda kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika sekta mbali mbali ikiwemo maji, huduma ya afya, miundombinu ya barabara na huduma za kijamii.

Kadhalika amewahimiwa wanawake kuendelea kushirikiana bega kwa bega katika kukijenga chama ili kiweze kuwa Hai na kuweka mikakati madhubuti ya kutumia fursa za mikopoo ambayo inatolewa na Halmashauri lengo ikiwa ni kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wiimbi la umasikini.

 Pia katika hatua nyingine akizungumza na wanachama ambao wamehudhulia katika sherehe za maadhimisho hayo amewakumbusha wazazii na walezi kuweka misingi imara kwa watoto wao kwa lengo la kudumisha hali ya amani na utulivu katika nchi yao na kuachana kabisa na tabia ya kufuata makundi mabaya ambayo hayana faida kabisa na nchi ya Tanzania.

                                            

Post a Comment

0 Comments