wakazi wa mbeya wavutiwa na msimu wa raha kamili na serengeti.

Msanii mahiri wa hip hop BOngo,aitwaye Roma akiwarusha vilivyo wakazi wa Mbeya jioni ya leo kwneye tamasha la Msimu wa raha kamili na serengeti,lililofanyika katika uwanja wa mpira wa sokoine.
Sam wa ukweli wakiwapagawisha baadhi ya wakazi wa Mbeya na kibao chake cha Sina Raha,kwenye uwanja wa Sokoine mjini Mbeya jioni ya leo,huku wakazi hao wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika tamasha hilo la Msimu wa raha kamili na Serengeti.
Mashabiki na wapenzi wa tamasha la Msimu wa raha kamili na serengeti wakiwa wamepagawa vilivyo jioni ya leo kwenye uwanja wa Sokoine,wakati wasanii mbalimbali walipotumbuiza.
Watu kibao kwenye tamasha la Msimu wa raha kamili na serengeti.
Wapenzi wa mfalme wa raha kamili wakijipatia vinywaji taratiibu huku wakifuatilia makamuzi ya wasanii mbalimbali waliokuwa wakitumbuiza jioni ya leo kwenye uwanja wa Sokoine,mjini Mbeya.
Staili mpya ya kiduku kutoka kwa wakazi wa Mbeya jioni ya leo.
Msanii mahiri na mmoja wa mabalozi wa Malaria hapa nchini,Mwasiti akiwaimbia wakazi wa Mbeya jioni ya leo wimbo wake wa sio kisa pombe kwenye tamasha la Msimu wa raha kamili na Serengeti.
Kutoka THT,Amin akiimba kwa hisia mbele ya wakazi kibao kutoka mjini Mbeya jioni ya leo.
Mkali mwingine wa hip hop Bongo,Godzilla akiwashushi mistari wakazi wa mbeya,jioni ya leo kwenye tamasha la Msimu wa raha kamili na Serengeti katika uwanja wa sokoine.
Beka Boy,Amin na Barnaba wakilishambulia jukwaa vilivyo
uwanja wa Sokoine jioni ya leo ilikuwa ni Shangwe tu mwanzo mwisho.
Barnaba na Lina kwa pamoja wakiwaburudisha wakazi wa Mbeya jioni ya leo kwenye uwanja wa Sokoine.
Lina akijiachia vilivyo na shabiki wake jukwaani.
Dj Choka akikamua kwenye mashine,huku mdau Adrew Kussaga akiyacheki kwa makini machejo ya Dj Choka a.k.a Mr Apetite.
Pichani ni wakazi kutoka sehemu mbalimbali ya mji wa Mbeya waliofika kuwashuhudia wasanii mbalimbali waliofika kuwatumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Msimu wa Raha kamili na Serengeti,lililofanyika katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Post a Comment

0 Comments