VODACOM MWANZA CYCCLE CHALLENGE 2010 KUTIMUA VUMBI NOVEMBA

Meneja Matukio Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa pamoja na Mkuu wa Udhamini Vodacom George Rwehumbiza wakionyesha nembo watakayotumia katika mashindano hayo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Baiskeli Tanzania Nazir Manji akizungumza katika mkutano huo.
Kutoka Kushoto ni Meneja Matukio wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa,akifuatiwa na Mkuu wa Udhamini Vodacom George Rwehumbiza Mwenyekiti wa Chama Cha Baiskeli Tanzania Nazir Manji na Mdau wa mchezo huo wakiwa katika Ukumbi wa Idara Ya Habari MAELEZO D ar es Salaam ambapo walitangaza tarehe ya mashindano hayo yatakayofanyiika kati ya Novemba 12 na 13 Jijini Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini leo Rwehumbiza alisema kwamba mashindano ya mwaka huu yameboresha zaidi ikiwa ni pamoja na upande wa zawadi na kuwaomba washiriki ambao ni waendesha baiskeli kujitokeza kwa wingi.Alisema mashindano hayo yatakuwa ya mbio za Kilomita 196 kwa wanaume, Kilomita 80 kwa wanawake na kwa upande wa walemavu wanaume watakimbia mwendo wa Kilomita 15 huku walemavu wa kike watakimbia Kilometa 10.
Washindi wa kila kundi watapewa zawadi ambazo zitatangazwa baadaye ambapo pia mashindano ya mwaka huu yamedhaminiwa kwa shilingi milioni 50."Shindano la mwaka huu la Mwanza Cycle Challenge litakuwa linafanyika kwa mara ya 5 huku likidhaminiwa na Vodacom Tanzania ambapo wadhamini wengine ni Alphatel, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Knight Support na SBC kupitia kinywaji chake cha PEPSI",."Shindano hili ni maalum kwa kukuza mchezo huu hapa nchini kwa lengo la kupata wawakilishi bora katika mashindano mbalimbali ya kimataifa" alisema Rwehumbiza.Wakati huohuo Mwenyekiti wa Chama Cha Baiskeli Tanzania (CHABATA) Nazir Manji ameomba uongozi wa Vodacom kuwekeza zaidi katika mchezo huo hata kama itakuwa ni mwakani kwa kuwapa nafasi wachezaji wenye umri mkubwa wawili (Seniors) na Chipukizi wawili (Juniors) kwa kuwagharamia katika mashindano ya Kimataifa mara wanapopata mwaliko. Manji amesema hivyo kufuatia kushindwa kwao kuliwakilisha Taifa kutokana na (CHABATA) kupoteza nafasi huizo kila mwaka kutokana na ukata mara wanapopata mialiko kila mwaka kutoka Chama Cha Mbio Za Baiskeli Duniani (UCI) kama ilivyotokea mwaka huu walipata mwaliko lakini wameshindwa kupeleka wawakilishi.

Post a Comment

0 Comments