Ndugu Wana Habari sisi Kampuni ya Abama Inc .yenye maskani yake Jijini Dar es Salaam, tunajishughulisha na uhamasishaji wa bidhaa mbalimbali na kuratibu matamasha mbalimbali ya burudani nchini.
Hivi katibuni Kampuni yetu ilipewa jukumu kuandaa uzinduzi wa albamu ya kundi la muziki dansi la Mapacha wa 3 linaloundwa na wanamuziki hawa mahiri nchini Jose Mara, Khalid Chuma na Kalala Junior.
Wanamuziki hawa mbali na kuwatumikia waajiri wao wao wamekuja na wazo la kuanzisha kundi lao nje ya bendi zao ambapo wana lengo la kujiongezea kipato huku albamu yao inakwenda kwa jina la 'Jasho La Mtu' itakayozinduliwa Ijumaa Oktoba 16 ndani ya Ukumbi wa Traventine Magomeni Dar es Salaam.
Uzinduzi huu umeandaliwa kimataifa ukiwa na lengo la kubadili sura na mwelekeo kwa wanamuziki hasa dansi nchini , pia Mapacha 3 waytatoa wito kwa wadau na wapenzi wa muziki kuja kwa wingi kuthibitisha uwezo walio nao na kile walichowaandalia siku hiyo.
Pia aliwataja wadhamini waliowawezesha kuwani Redio 88.4 Clouds FM na Clouds Redio, Channel Ten, DTV, C2C, Magic FM, Mama Ife Entertainment, Gazeti la Risasi, Eventilities, Valley Springs Limited, Lulu Quality Cosmetics, Amos Collection, Rutinga Communication Agency na Zizzou Fashion.
0 Comments