Skauti wa Tanzania Kuadhimisha Jamboree ya 53 ya Kimataifa Mawasiliano na Redio

Skauti wa Tanzania wataungana na skauti wengine duniani kuadhimisha Jamboree ya Hewani ya KimataifaJamboree ya Hewani ya Kimataifa ni shughuli ambayo huadhimishwa kila mwaka mwezi Oktoba ambapo skauti huwasiliana kutoka nchi moja hadi nyingine kwa kutumia vifaa vya Mawasiliano ya Radio. (Amateur Radio).Huu ni mwaka wa 53 tangu tukio hilo lianze kuadhimishwa duniani pote. Na Skauti wa Tanzania watapiga kambi rasmi katika uwanja wa Makao Makuu ya Chama cha Skauti Tanzania barabara ya Malik upanga jijini D’salaam. Kuanzia Oktoba 15 hadi 17 mwaka huu.
Sherehe rasmi za ufunguzi zimepangwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 16 Oktoba 2010 saa 4.00 asubuhi, ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Kamanda Mohamed Mpinga.
Sambamba na shughuli hiyo ya Mawasiliano kwa njia ya Radio, Skauti pia watawasiliana na skauti wengine duniani kwa kutumia Mtandao wa Internet. Jamboree On The Internet.([JOTI) Jumla ya Skauti zaidi ya 1000 kutoka mkoa wa DSM na mikoa ya jirani , wanatarajia kushiriki shughuli hiyo ambayo pia Wazazi na Walezi wa Maskauti, pamoja na Vyama marafiki wa Uskauti wamealikwa kuhudhuria.
Habari hii imetolewa na Kamishna Mkuu wa Chama Cha Maskauti nchini Laurence Mhomwa.

Post a Comment

0 Comments