Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Ambwene Yessayah ‘AY’ Jumapili Septemba 10 anatarajiwa kupagawisha kwa shoo ya aina yake kwenye klabu ya kisasa ya kimataifa, Club Bilicanas jijini Dar es Salaam.Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, AY aliwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi ili kupata burudani ya nguvu.Msanii huyo ambaye anatamba hivi sasa na vibao kama ‘Habari Ndiyo Hio’ na ‘Usije Mjini’ ambao ameimba na Khamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’, amezidi kujipambanua kimataifa, ambako hivi karibuni sambamba na msanii kutoka Trinidad na Tobago, Ms Trinity walikwenda nchini Uganda na kurekodi video yao mpya.AY alisema, wimbo huo waliorekodi katika studio ya B.Hits ya jijini Dar es Salaam, video yake ilifanyiwa ndani ya Jiji la Kampala chini ya mwongozaji Donald kutoka Dedac Production.Akizungumzia onyesho lake la Jumapili linalofahamika kama ‘Stars Nite AY’, alisema amejiandaa vya kutosha hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi siku hiyo, ili kupata burudani ya kisasa.Katika mipango yake zaidi, AY anatanabaisha kuwa, anatarajia kurekodi nyimbo nyingine na wasanii wakubwa kama Mjamaica Sean Kingston, mwenye msakani yake nchini Marekani na J Martins wa Nigeria.
DC Mpogolo apokea taarifa uboreshaji Shule za Msingi Olympio Diamond,
Zanaki Bunge, Mzizima na Kisutu
-
Na MWANDISHI WETU
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amepokea taarifa maalumu ya
mikakati ya uboreshaji wa Shule za Msingi Olympio Diamond, Zana...
7 hours ago
0 Comments