JAMANI HII SIYO SHEPU YA KICHINA NDIVYO ALIVYO

EFRANCIYA MANGII

Nyota yake ilionekana katika shindano la Maisha Plus 2009, lakini pia akajiongezea umaarufu kutokana na umbo lake ‘mashaallah’ kisha aliposhiriki kwenye filamu mbalimbali. Anaitwa Efranciya Mangii.

TQ: Mambo vipi mrembo? Naamini uko fresh, tayari kuchonga na Mzee wa TQ. Hebu tuambie, kabla ya kushiriki Shindano la Maisha Plus ulikuwa unafanya nini?

Efranciya: Nilikuwa nafanya mambo yangu binafsi ambayo sioni umuhimu wa kuyaanika hapa, kwa kifupi nilikuwa ‘home’ tu.

TQ: Mshindi katika shindano hilo alijipatia kitita cha shilingi milioni 10, wewe umefaidika nini na shindano hilo ukiachilia mbali kuuza nyago kwenye runinga?

Efranciya: Zaidi ya kuuza nyago na kujipatia umaarufu pia nimejifunza namna ya kuishi na watu katika mazingira tofauti na yale niliyoyazoea ya kuishi mjini.

TQ: Kuna tetesi kwamba umbo lako la ubonge limekusaidia sana kupenya katika mashindano hayo, unadhani maneno haya yana ukweli wowote?

Efranciya: Naweza kusema kuna ukweli kuhusu hilo maana hata siku wananifanyia usaili walikuwa wakiniambia nigeuke nyuma kisha wanachekelea .

TQ: Kuna jaji yeyote alikutongoza kwa kudatishwa na umbile lako?

Efranciya: Aka! Sijatongozwa na jaji yeyote ingawa umbile langu liliwaacha hoi. Kijijini aliyenitongoza ni mshiriki mwenzangu aitwaye Maulid tu. Huyu alinifukuzia mno lakini hakuambulia kitu kwani nilikuwa na mpenzi wangu.

TQ: Tuachane na Maisha Plus, wewe kama Efranciya ni kipi unachotarajia kukifanya au unachokifanya sasa?

Efranciya: Kwasasa nimejikita kwenye uigizaji wa filamu, lengo ni kuja kuwa msanii maarufu kama vile Irene Uwoya na wengineo. Naamini siku moja ndoto yangu itatimia.

TQ: Ni kipi kinachokukosesha amani katika maisha yako ya kila siku?

Efranciya:Yaani watu wanavyonidhihaki kuhusu umbile langu. Kibaya zaidi wanadai nimetumia dawa za Kichina za kuongeza makalio wakati si kweli, haya ni majaaliwa ya Mungu hivyo washindwe na walegee.

TQ: Ni kitu gani katika maisha yako utafurahi endapo kitatimia?

Efranciya: Kutimiza malengo yangu nikiamini kwamba yakitimia hata maisha yangu yatakuwa ya furaha zaidi.

TQ: Umeolewa wewe?

Efranciya: Sijaolewa wala sijafikiria kitu kama hicho ila nina mpenzi wangu tunayependana sana.

TQ: Mpenzi wako ni Masele Chapombe ambaye hivi karibuni ulimuanika au una mwingine? Maana nyie hamkawii.

Efranciya:Aaah,eeeh mbona…..!

TQ: Naona unapata kigugumizi kuzungumzia hilo, anyway tugeukie kwenye suala la misosi, nasikia unapenda sana kula na kwamba ifikapo muda wa maakuli ‘usistaduu’ unauweka pembeni kuna ukweli wowote?

Efrancyia: Jamani maswali gani sasa hayo? Hivi kuna mtu asiyependa kula kweli? Yes kula ni sehemu ya maisha yangu.

Post a Comment

0 Comments