WAKILISHA TAMASHA LILILOWAKUMBUSHA VIJANA KUPIGA KURA OKTOBA 31

Banana Zorro kushoto akiimba pamoja na baba yake Mzee Zahir Ally Zoro katika tamasha la kuhamasisha vijana kwenda kupiga kura ifikapo Oktoba 31 kwa ajili ya kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani.
Mwanamuziki Fid Q kulia na MwanaFA nao walikuwepo katika tamasha hilo wakiwakilisha vijana na kuwahamasisha juu ya kupiga kura kwenye uchaguzimkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Oktoba 31 mwaka huu.(Picha zote kutoka Fullshangwe Blogspot) Kutoka kulia ni wanamuziki Mwasiti, Keisha na Mahunda wakipozi kwa picha wakati wa tamasha la Wakilisha 31, 2010 lililofanyika kwenye viwanja vya Biafra Kinondobi jana.
Umati Mkubwa wa mashabiki wakifuatilia kwa makini wakati wasanii mbalimbali walipokuwa wakiimba kwenye tamasha la kuhamasisha vijana kwenda kupiga kura Oktoba 31 mwaka huu.WAKILISHA 31, 2010 ni Tamasha lenye lengo la kuhamasisha vijana kwa ajili ya kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu nchini kote.
Tamasha hilo limefanyika jana Jumapili kwenye viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es salaam likishirikisha wasanii mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania huku likifana kwa kiwango cha hali ya juu. Kitu kinachoonyesha kwamba ujumbe umefika kwa vijana wote waliohudhuria katika tamasha hilo hivyo bila shaka watatoka na kwenda kupiga kura ifikapo Oktoba 31 kama walivyokumbushwa kupitia ujumbe uliokuwa ukitolewa kupitia jukwaa hilo kwa njia ya muziki.

Post a Comment

0 Comments