Na Juma Kasesa
Afya ya Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam, ‘Super Coach’ Syllersaid Said Mziray imezidi kudhoofika baada ya kuwekewa mipira kwa ajili kumsaidia kupumua.
Mziray Kocha aliyeipa Tanzania Bara mafanikio kwa kuiwezesha kutwaa kombe la Chalenji mara ya mwisho 1994 jijini Nairobi, amelazwa katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU).
Mwandishi wa Habari hizi ambaye alifanikiwa kuvuka vigingi vilivyowekwa na familia Mziray kuzuia waandishi wa Habari kumuona kocha huyo,na kuingia chumba alicholazwa, alishuhudia Mziray akizungumza kwa shida huku akiwa amewekewa mipira hiyo kwa ajili kumsaidia kupumua.
Kwa siku kadhaa tangu kocha huyo ameanza kuugua na kulazwa katika Hospitali ya Regency kabla ya kuhamishiwa Aga Khan juzi ameshazushiwa kifo mara kadhaa na familia yake kukanusha taarifa huku ikigoma kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari ambavyo ni mdau mkubwa wa kocha huyo kuhusu hali yake kiafya.
Aidha katika hatua nyingine mwandishi wa habari hizi aliwashuhudia maofisa wa Serikali wakiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo Tanzania Juliana Yassoda ambaye inasemekana alisoma pamoja na Mziray, na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania, Seth Kamhanda wakiwa Hospitalini hapo kwa lengo la kumjulia hali kocha huyo.
Mziray alijiunga na Simba hivi karibuni kwa lenngo la kuimarisha benchi la Ufundi la timu hiyo ambayo, alishindwa kuingoza katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya watani zake wa jadi Yanga ulipigwa jijini Mwanza wiki iliyopita na Simba kuchezea kichapo cha bao 1-0 lililofungwa Jerson Tegete katika dakika ya 71 katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza Jumamosi iliyopiata.
Rais Samia anawajali watu wenye Mahitaji Maalum: Naibu Waziri Mwanaidi
-
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
Tanzania Mhe Mwanaidi Ali Khamis akiwa katika picha ya pamoja na Watoto wa
Nyumba ...
8 hours ago
0 Comments