Mwisho Mwampamba mara baada ya kuwasili jana jionikwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere Dar es Salaam akitoka Afrika Kusini kwa Shirika la Ndege la SAA ambako alishiriki shindano la Big Brother Africa All Stars na kushika nafasi ya tatu huku mshiriki Uti kutoka Nigeria akiibuka mshindi na kupata zawadi ya kitita cha Dola 200,000 za Kimarekani. Kwa mujibu wa uongozi wa Multichoice leo Mwisho, anatarajiwa kutembelea vyombo mbalimbali vya habari ambako pia ataeleza mambo mbalimbali yaliyojiri kwa muda wote wa siku 91 alizokaa ndani ya jumba Big Brother pamoja na washiriki wenzake wakati kesho ameandaliwa mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika Jijini Dar es salaam .(Picha na Blog ya Fullshangwe).
FEZA BOYS YAFAULISHA KWA ALAMA A; WANAFUNZI WOTE WAPATA MATOKEO MAZURI
KIDATO CHA NNE
-
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa
Kidato cha Nne, huku baadhi ya wanafunzi wakifutiwa matokeo yao kutokana na
makosa...
17 minutes ago
0 Comments