Watoto wasio na makazi maalum wanahitaji msaada wako wa hali na mali

Mratibu na Ofisa Uhusiano wa Kituo Cha 'New Hope Family Street Children', Andrew Chale wakwanza kulia akikabidhi taa kubwa za chemri pamoja na vyombo mbalimbali kwa niaba ya Uongozi wa Vijana wa Kanisa la St.Columbus la Upanga Jijini Dar es Salaam.Kanisa hilo kupitia kwa Madam Nuru lilitoa vitu hivyo kwa ajili ya matumizi.
Viongozi wa New Hope Family Street Children, kushoto Mwenyekiti Omary Rajabu, katikati Hashimu Yuphu na Mlinzi wa watoto hao kwa mitaani pamoja na kituo hicho,Tizzo.Kwa niaba ya wenzao waomba masaada wako.Kituo hiki cha watoto hawa mpaka sasa kina watoto 25 ambapo watoto wengi wao awali walikuwa wakiishi kwenye mazingira magumu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na kujishughulisha na uombaji yaani ombaomba pamoja na kuokota makopo na vyuma chakavu.Kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia, watoto hao wenyewe kwa pamoja waliamua kutafuta wafadhili ili wawe sehemu moja na kupatiwa nyumba hiyo ya kupanga.Maitaji wanayotaka kwa sasa ni CHAKULA :mchele/unga/sukari/maharagwe na misaada mingine.

Post a Comment

0 Comments