TPF Net PWANI WAKABIDHI MSAADA KWA WANAFUNZI WA KIKE SEKONDARI YA MANDELA


 Mwenyekiti wa TPF Net Mkoa wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Batseba Kassanga leo  18  Oktoba ,2024  amewaongoza 
Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali kutoa msaada wa mashati 70 kwa wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Mandela iliyopo Wilaya ya Kipolisi Chalinze ambao waliunguliwa na bweni lao 12,Oktoba ,2024.
Sehemu ya mabaki ya vitanda na vifaa vya wanafunzi vilivyoungua.
Akikabidhi msaada huo SSP Batseba alitoa pole kwa uongozi wa shule na wanafunzi hao kwa maafa yaliyowafika na kuwataka waichukulie kama ajali na waendelee kuchukua tahadhari ya majanga kama hayo.
Kwa upande wake Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chalinze Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Sophia Lyidenge amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii zaidi kwani wana  kipindi kifupi kuelekea mitihani yao ya mwisho na muda watakaokuwa nyumbani wakisubiri matokeo waendelee kuwa na tabia njema ili wasije kuharibu ndoto zao.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mwanafunzi Neema Abdallah aliwashukuru wana mtandao wa TPF Net Mkoa wa Pwani kwa msaada waliyowapatia na waliahidi kutowaangusha kwa kufanya vizuri kwenye mitihani yao.
Aidha Mkuu wa Shule hiyo ya Wasichana Mandela,Bi. Regina Ngereza alitoa pongezi kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa namna walivyoonesha ushirikiano kwao tangu walivyopokea taarifa ya kuungua kwa bweni hilo na aliwaomba waendelee kuwa na moyo huo kwa jamii.

Post a Comment

0 Comments