TAKUKURU PWANI YAWABANA WAAJIRI KUCHANGIA NSSF YAOKOA BIL.1.5

 


Kibaha, Pwani 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani imefanikisha kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.5 ambayo ni michango ya wafanyakazi kupitia Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kutoka kwa waajiri walioshindwa kuingiza michango ya wafanyakazi.

Hayo yamesemwa leo
 na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Alli Sadiki  alipozungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mjini Kibaha wakati akitoa taarifa ya kipindi cha Julai hadi Septemba 2024.

Sadiki amesema kuwa TAKUKURU iliingilia kati katika mfumo wa ukusanyaji wa michango ya waajiri ambao walikuwa hawapeleki michango ya waajiriwa kupitia NSSF.

"Meneja wa NSSF Pwani alilalamikia upotevu wa makusanyo kama michango ya waajiri inayosababisha upotevu wa fedha na usumbufu kwa wastaafu kutolipwa mafao yao kwa wakati,"amesema Sadiki.

Aidha amesema kuwa uzuiaji huo umefanyika baada ya kuwatafuta waajiri  77 ambao walikuwa na deni la michango ya Shilingi bilioni 7.5 ambapo Takukuru imeingilia kati kuhusu ukusanyaji wa michango ndipo wadaiwa na NSSF walikubaliana ifikapo Julai 24 mwaka huu walipe deni hilo kwa asilimia 20.

"Wakati huohuo  TAKUKURU  wamefanya uchambuzi  wa mfumo mmoja  katika  eneo la  upatikanaji  wa huduma  na dawa  kwa wagonjwa  wanaotumia  bima  ya NHIF  kwenye  hospitali, vituo vya afya  na zahanati  za serikali na binafsi katika  Halmashauri  ya Mji Kibaha. Katika chambuzi huu wa mfumo uliofanyika mapungufu  yaliyobainika  na tayari hatua  zimechukuliwa" amesema Sadiki.
Ameongeza  kwa kusema kuwa  katika eneo la uzuiaji  rushwa  wamefanya kazi ya ufuatiliaji  miradi 53 ya maendeleo  yenye thamani ya Bil.14,490,667,779.32 katika sekta za afya, elimu, maji na barabara. 

Sadiki amesema kuwa TAKUKURU Mkoa wa Pwani wamejipanga kuendelea  kutoa elimu madhara  ya rushwa katika  uchaguzi  kupitia semina,mikutano  ya hadhara na vipindi vya redio ili kuwafikia wadau wote wanaoshiriki  kwenye uchaguzi. Lengo ni kushiriki uchaguzi usiokuwa na  vitendo vya  rushwa,pia tutaendele kufanya udhibiti  wa mapato ya serikali  na usimamizi  wa rasilimali  za umma ikowq ni pamoja na ufuatiliaji  wa fedha zinazotolewa na serikali  kwa ajili ya kutekeleza  miradi ya maendeleo tutaendelea  kupokea  taarifa za vitendo  vya rushwa kufanya uchunguzi na kufukisha watuhumiwa  Mahakamani.

TAKUKURU Mkoa wa Pwani imetoa wito kwa wananchi kuendelea  kuunga  mkono jitihada  za mapambano  dhidi  ya rushwa  kwa kufichua  wale wote wanaoshiriki  kufanya  vitendo vya rushwa kwa kutoa taarufa  sahihi  zitakazowezesha  kuwachukulia  hatua  wahusika hasa katika  kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.

"Nawaasa  wananchi kufuata  sheria kanuni na taratibu  zilizowekwa ili kuwa salama na kuepuka migogoro  yenye kuleta  viashiria vya rushwa"amesema Sadiki.

Amesema kuwa  katika kipindi cha Julai na Septemba TAKUKURU  wamepokea malalamiko 88 kati ya hayo malalamiko 68 yalihusu rushwa na taarifa hizo zimeshughulikiwa  kwa mujibu wa sheria  kwa kuanzisha  uchunguzi ambao upo katika hatua mbalimbali za uchunguzi. 

"Taarifa 20 zilizobaki ambazo hazikuhusu rushwa zimeshughulikiwa  kwa njia ya  uelimishaji,uzuiaji, ushauri  na kuhamishiwa idara ingine. Taarifa  hizo zimepokelewa  kwa mchanganuo ufuatao TAMISEMI 20  Mifugo/Uvuvi 4,Elimu 21,Polisi 5,Ardhi 6,Fedha 2,Maji1,Mahakama 4 ,binafsi 2,Misitu2,AMCOS1,Usafirishaji 2 Viwanda 1,Vyama vya wafanyakazi 1,Ujenzi 2,Afya7,Siasa 1,Manunuzi 1 na Maendeleo ya Jamii 2 pia tumefungua kesi mpya 22 Mahakamani  huku kesi 12 washtakiwa wametiwa hatiani"amesema Sadiki.

Post a Comment

0 Comments