Ofisa
wa Matibabu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Yasinta
Shibola akitoa ufafanuzi kwa watu mbambali waliotembelea banda la NSSF
wakati wa maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar
es Salaam leo ambapo NSSF ni moja ya taasisi zinazoshiriki katika
maonesho hayo.
Baadhi ya watu mbalimbali wakipata maelezo ya huduma zinazotolewa na Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na hasa huduma ya mafao ya matibabu
iliwafutia watu wengi, wakati wa maonesho ya Huduma za Hospitali ya
Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Ofisa
Uhusiano Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Maife Kapinga akifafanua jambo kuhusu huduma ya mafao ya
matibabu wakati wa maonesho ya Huduma za Hospitali ya Taifa Muhimbili
jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya watu waliojitokeza katika banda la NSSF wakipata maelezo ya huduma mbalimbali za NSSF.
Na Mwandishi Wetu
WATANZANIA wametakiwa kujiunga na Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF), ili kufaidika na huduma za bure katika mafao yanayotolewa na
shirika hilo.
Wito huo umetolewa leo na Ofisa wa matibabu wa NSSF, Yasinta
Shibola, jijini Dar es salaam katika maonesho ya siku tatu ya Muhimbili
kutimiza miaka 13 toka kupandishwa hadhi ya kuwa hospitali ya Taifa tangu mwaka
2000.
Shibola alisema kuwa NSSF hawatoi mafao ya kustaafu pekee bali
wana mafao mengine ambayo hutolewa bure kwa mwanachama aliyejiunga na mfuko
huo.
“Mafao yetu yamejikita kusaidia wateja wa sekta binafsi na wa
serikali, lakini pia hata wale wanaofanya kazi kwa kujitegemea kama atakuwa
mwanachama wetu atapatiwa fao hilo kama wengine tena katika hospitali
atakayochagua yeye mwenyewe katika zile ambazo tumeingia nazo mkataba na kupewa
fao hilo kama wengine wote, hakuna upendeleo hapo,”alisema
Naye Ofisa habari wa NSSF, Maife Kapinga, alisema kuwa fao la
matibabu (SHIB) ni bure na linahudumia watu wanne katika familia moja.
Aidha alisema kuwa maonesho hayo yamekata kiu ya wafanyakazi wa
Muhimbili pamoja na wagonjwa kwani wengi walikuwa hawana elimu ya namna shirika
hilo linavyofanya kazi japo ni wanachama.
Kapinga alitoa wito kwa watanzania kujiunga na shirika hilo ili
wafaidike na mafao yanatolewa bure.
0 Comments