Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Theresia Everist Kyara ambaye alikua mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alifafanua jambo kuhusu mbio hizo.
Mwakilishi kutoka Hospitali ya Rufaa Tumbi Mkoa wa Pwani Judith Mwinuka akielezea namna watakavyo shiriki kwenye mbio hizo za 'Coast City Marathon '.ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za afya .
Mwinuka amesema kuwa wanatoa ahadi ya kushiriki kwa wingi sambamba na kutoka huduma za afya kwa washiriki kama ilivyokua kwenye msimu uliopita.
Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Tigo Omary Hamza, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Dkt Frank Mhamba na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Theresia Everist Kyara walipozungumza na waandishi wa habari hawapo pichani leo tarehe 11 Novemba, 2024.
Balozi wa mbio hizo Twaha Ambiere akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika leo tarehe 11 Novemba ,2024 Kibaha Mkoani Pwani.
Balozi wa mbio hizo Twaha Ambiere akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika leo tarehe 11 Novemba ,2024 Kibaha Mkoani Pwani.
Balozi wa mbio hizo hizo Twaha Ambiere amesema kuwa kutakua na mbio za watoto 2.5Km 5Km,10Km,15 Km na 21Km pia amesisitiza usajili ni kiasi cha 35, 000 kwa kila mmoja ambapo mshiriki atapata medali ,fulana pamoja na riboni ya mkononi.
Amesema kwa mbio hizo za Coast City Marathon zinafanyika kwa mara ya tatu sasa huku zikiwa zinachagiza kukuza sekta ya michezo na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali kwenye jamii.
Ambiere, ametoa hamasa kwa wadau kujitokeza kwa wingi kujisajili ili waweze kushiriki kikamilifu.
Mbio hizo zimedhaminiwa na CRDB, NSSF, TIGO, DAVISA &SHIRT LIFE na wengine wengi.
Kutoka kushoto Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Theresia Everist Kyara akikabidhiwa jezi na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio za Coast City Marathon Dkt.Frank Mhamba kwenye uzinduzi uliofanyika leo tarehe 11 Novemba 2024 Kibaha ,Mkoani Pwani
Kibaha,Pwani
Ikiwa imezoeleka kuwa kwenye mbio kunakua na vituo vya kutoa maji ya kunywa kwa wakimbiaji imekua tofauti kwa waratibu wa Coast City Marathon wamesema kuwa wao watatoa maji ya dafu na supu ya pweza.
Katika maboresho ya mbio za mwaka huu Coast City Marathon tumeamua kunogesha kwa kuwa na vituo vitakavyokua vinatoa maji ya madafu na supu ya pweza kwa wakimbiaji ikiwa ni katika kuenzi utamaduni wa Mkoa wa Pwani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo ya taehe 11, Novemba 2024 kwenye uzinduzi rasmi wa mbio hizo Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Dkt. Frank Mhamba amesema kuwa mbio hizo zitafanyika Novemba 30 mwaka huu.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Theresia Everist Kyara amesema kuwa wote tunafahamu kuwa serikali yetu inatumia fedha nyingi katika kupambana na magonjwa yasiyo ambukiza hivyo natoa wito kwa wananchi wote wa Kibaha na amaeneo jirani na Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye mbio hizi na kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi.
Kyara amesema kuwa kiasi cha fedha zitakazopatikana zitakwenda kuboresha miundombinu ya Shule ya Msingi Pangani kwa kujenga jengo la Utawala ambapo shule hiyo ipo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
0 Comments