UJENZI KIWANDA CHA KOROSHO KISARAWE UKAMILIKE MAPEMA-DC MAGOTI


Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Kisarawe  Beatrice  Dominic akiwa kwenye picha ya pamoja na  Mkandarasi Ahmed  Mussa  wa Mohammed Limited Builders  Limited  wakuonesha mikataba waliyosaini ya ujenzi wa Kiwanda cha Korosho na aliyesimama katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe Zuberi Kizwezwe
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Tito Magoti  pichani juu ametoa rai ya kukamilika kwa  ujenzi wa kiwanda cha Korosho Wilayani Kisarawe  haraka iwezekanavyo. 

Rai hiyo imetolewa  na DC Magoti mara baada ya kushuhudia  utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa Kiwanda hicho  cha Korosho ambapo pia alikua mgeni rasmi.

Aidha DC Magoti amemwambia Mkandarasi  wa unenzi huo kuwa   unjenzi ufanyike usiku na mchana ili msimu ujao wa Korosho wakulima wa Kisarawe wasihangaike kusafirisha korosho zao kupeleka Kibaha na Mkuranga kwa  ajili  ya kubanguliwa nakuwaongezea gharama wakulima kwa kukatwa fedha za ziada hivyo ujenzi wa Kiwanda hicho   utawasaidia kupunguza  gharama  wakulima na baada ya ujenzi wataona faida ya zao hilo.

"Ujenzi wa Kiwanda hiki utaleta maendeleo  ndani ya Kisarawe, Wilaya hii ipo kwa zaidi ya miaka 80 hatuna Hospitali  kubwa,Kituo kikubwa cha Polisi,hatuna Idara ya Uhamiaji  kwa kuona hilo Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amepanga kutuletea  zaidi ya Bil.12 ambazo zitakuja kuleta maendeleo  hivyo nawaasa wananchi na wote ambao mko kwenye maeneo ambayo fedha hizi za miradi mbalimbali zitapita nawaasa mziogope fedha za serikali na endapo  itabainika  unajishirikisha  kuhujumu kuna kitu kinaitwa  udava udava kitakukuta"amesema DC Magoti .

DC Magoti amesema hayo 18 Oktoba 2024 alipokuwa mgeni  rasmi  kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa  jengo la kiwanda  cha Korosho Kisarawe Mkoani Pwani. 

Ujenzi wa Kiwanda  hicho kitajengwa na  Mohammed  Builders  Limited  na kusinamiwa na Mkandarasi  Ammar  Janoowala kiwanda hicho kitajengwa kwa gharama  ya Bi.2.5

 Amesema  kuwa Kiwanda hicho kitakua na uwezo wa kubangua tani 3 hadi 4 kwa siku moja na ujenzi huo unatarajiwa kuanza Novemba mosi  mwaka huu

Mkandarasi  Ahmed Mussa wa Kampuni ya Mohammed Builders  Limited amesema kuwa  anathibitisha  ujenzi wa Kiwanda hicho utakamilika ndani ya mwaka mmoja.

Wakati huohuo  DC Magoti amesema kuwa katika kukuza uchumi wa wakaazi wa Kisarawe pia watajenga soko la mihogo ili mkulima wa zao hilo aweze kufaidi na kuona matunda yake tofauti  na ilivyo  hivi sasa ambapo wakulima wanauza bei kandamizi  na za  kinyonge  wanazopangiwa na madalali 

Post a Comment

0 Comments