WAKILI MSOMI MAJALA AUAWA KIKATILI NA MTOTO WAKE

Aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Michezo Tanzani Wakili Msomi Riziki Majala pichani juu amefariki dunia kwa kuuawa kutokana kudaiwa kupigwa na mtoto wake wa kwanza wa  kiume  aliyefahamika kwa jina la Juma  Riziki Majala anayekadiriwa kuwa na umri kati ya (23na 24).

Akithibitisha  kutokea kwa tukio hilo  Mjumbe wa Mtaa wa Mkuza Kibaha  Salumu Abasi  Mtowela amesema kuwa  mara baada ya kupata  taarifa za tukio hilo leo 18 Oktoba 2024 majira ya asubuhi  alikwenda kutoa taarifa Kituo kidogo Cha Polisi Kwa Matiasi alipofika Kituoni hapo tayari Polisi walishapata  taarifa   za mauaji ya Majala.

Aidha  wakaondoka na Askari  kwenda nyumbani kwa marehemu  Majala na  walipoingia ndani wamemkuta Juma akiwa amekaa pembeni ya mwili wa baba yake na  nguo zilizokuwa na damu zikiwa zimewekwa kwenye ndoo hali iliyoashiria kwamba alipiga deki kufuta damu huku mwili wa marehemu ukiwa umelala chini sakafuni na  ukivuja  damu.
  Polisi wamemchukua  Juma  na  anashikiliwa na Kituo  Cha Polisi Mjimdogo Kibaha  Mkoani Pwani. 

Wakati huohuo  mpwa wa marehemu  Wakili Msomi Majala aliyehitambulisha  kwa majina ya Zuhura  Salum Seif  amesema yeye ndiye aliyezungumza na marehemu kwa mara ya amwisho jana usiku  majira ya saa tatu na nusu ambapo mpwa huyo alimpigia mjomba wake ili wajadili mustakabali wa kesi yake ya mirathi ambayo marehemu  Majala alikuwa Wakili wake  amesema.
" Majira ya sa nne usiku 17,Oktoba ,2024 nilimpigia simu mjomba na tukawa tunajadili mwenendo wa kesi yangu ya mirathi ambayo iko Mahakama ya Temeke yeye ndiye alikuwa Wakili wangu ndipo nikasikia sauti ya Juma ambaye ni mtoto mkubwa wa mjomba anasema  wewe mzee  nipe pesa  mimi nataka kwenda Bukene kwa sauti ya ukali baada yakusikia hayo maneno nikamwambia mjomba  ampe simu  niongee naye ili anipe namba nimtumie hiyo pesa anayohitaji sababu nilimsikia mjomba  akimjibu kuwa haba pesa  pia nikamsikia  Juma akisema hataki kuongea na mtu yeyote  yeye anataka pesa tu ndipo mjomba akaniambia nikate simu tutaongea baadaye au kesho na baada ya hapo leo asubuhi  18 Oktoba ,2024 nikakuta namba ya mjomba imenipigia niliipiga sana majira ya saa mojaasubuhi wakati huo mimi nilikua nje nilipoona hivyo nikapiga sana  lakini haikuwa na  majibu ndipo nikatuma ujumbe mfupi mmeamkaje huko mjomba nao  haukujibiwa nikapiga tena sumu ndipo Juma akapokea simu akasema babake amefariki nikamuuliza ilikuwaje akasema,
 yeye alitoka jana (17 ,Oktoba,2024)  usiku alikwenda The Game Bar iko kwa Matiasi akarudi usiku alipofungua mlango ukawa mzito alipousukuma akakuta babake amefariki "niliposikia hivyo nikamwambia Juma kweli umemuua babako kwa sababu ya pesa  akasema hajaua ndipo nilipowapigia ndugu zangu wanaoishi maeneo jirani na kwa mjomba  nikawaambia waende kuhakikisha na walipofika wakanieleza hali halisi  nimawaambia wasiingie ndani waende kutoa taarifa kituo cha Polisi, amesema Zuhura.

Wakati huohuo Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Pwani Muhudhwari Msuya anatarajia  kutoa taarifa kamili  ya tukio hilo kesho 19,Oktoba ,2024.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika  Hospitali ya Rufaa Tumbi  Mkoa wa Pwani.

Post a Comment

0 Comments