Tamasha la Wanyamwezi & Wasukuma lafika patamu

Mratibu Kadata Kawesela Kusula pichani amesema mambo ya maandalizi ta Tamashilo ambalo linatarajiwa kujaa msisimko wa hali ya juu yanakwenda vizuri. Tamasha hilo limepangwa kufanyika katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam.Aidha katika Tamasha hilo kutakuwa na ngoma za aina 2 ambazo ni ngoma ya Kinyamwezi inayofahamika kwa jina la Hiari ya Moyo mtindo ulioasisiwa na Hayati Sale Ramadhan Muinamila hivyo wadau watakumbushwa enzi za uhai wake mzee huyo aliyekuwa na upara ambapo mzuka ukimpanda alikuwa akinogesha kwa kupiga sarakasi. Na kwa upade wa kabila la Wasukuma wadau wa ngoma za asili wataonyesha umahiri kucheza na nyoka kwa Kiswahili ngoma hiyo tunaita Ubogobogo na Bugobogo kwa Kisukuma mdau kumbuka nyoka hawatakosekana siku hiyo katika viwanja hivyo kaa mkao wa kucheza na Chatu.Tamasha hilo limepangwa kufanyika Novemba 27 ambako kutafanyika kongamano na 28 ndiyo itakuwa siku ya kilele .Mbali ya ngoma pia kutakuwa na maonyesho ya vyakula vya asili ya makabila hayo, kama mboga aina ya nsansa za Nansolele na Ntwili, bila kusahau Nswalu, Matobholwa.Katika kongamano wadau watazungumzia namna ya kufufua utamaduni mila na desturi za makabila hayo mawili ikiwemo ngoma za jadi ambazo zimeshakufa.Wageni na viongozi wa ngazi za juu serikalini wanatarajiwa kuhudhuria tamasha hili.Habari hii ni kwa mujibu wa Kadata aliyezungumza na blog hii leo.

Post a Comment

0 Comments