Katika Picha ya pamoja baada ya mgeni rasmi kumaliza wajibu wake na kahidi kuwa pamoja nasi wakati wowote ambapo Chama Cha Waandishi wa Michezo na Burudani TASWA watakapo muhitaji. Semina hiyo ya siku mbili itamalizika kesho ambapo kutakwua na mwendelezo wa mada ya nne hadi ya saba. Kwa mujibu wa ratiba inaonyesha kuwa Mada ya nne itatolewa na Leslie Liunda, mada ya tano itatolewa na kocha wa mchezo wa Gofu, mada ya sita itahusu mchezo wa Volleyball wakati mada ya saba na itakayofunga semina hiyo itatolewa na Mwenyekiti wa MISA Ayoub Rioba na baada ya hapo Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto atamkaribisha mgeni rasmi kufunga semina na kuagana kwa ujuma.
Damas Ndumalu akijinafasi katika mlo wa mchana.
Damas Ndumalu akijinafasi katika mlo wa mchana.
Mkongwe Salim Said Salim(Journalist/Media Consultant (DW/RFI) mwenye maskani yake Zanzibar akijinafasi katika mlo wa mchana mara baada ya kuwakilisha mada.
Alfred Lucas a.k.a 'Brother Maps' kutoka gazeti la Mwanahalisi, Elius Kambili Championi na Said Kilumanga wa Channel Ten wakiwa makini.
Mwanasheria Damas Ndumalu akitoa mada ya Defamation,Exclusivity, Fair Use na nyinginezo.
Mwani Nyagasa kutoka gazeti la The African a.k.a Mmaushka akijisajili.
Dina Ismail akijisajili mara baada ya kufika kwenye chumba cha semina.Pia mtembelee latika http://www.mamapipiro.blogspot.com/.
Kutoka Kushoto Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto ,aliyekuwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Habari na Michezo nchini Joel Nkaya Bendera ambaye ndiye alifungua rasmi semina hiyo ya siku mbili na kutoa wito kwa waandishi wa habari za michezo kuwa na weledi ikiwa ni pamoja na kusoma na kufahamu kanuni za michezo yote ambazo wanaandika habari zake kila siku, na kusisitiza kwamba fani ya uandishi wa habari ni muhimu katika jamii na kuwataka Watanzania wazingatie katika michezo na kuacha kasumba ya kukesha bar na kwenye Pub ikiwa ni pamoja na kuacha anasa zisizo faa kwani ndizo zinzchangia mfumuko wa magonjwa mbalimbali.Pia amewataka wanahabari kuacha kuandika habari kwa ushabiki.Semina hiyo inaendelea kesho kwenye ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni Dar es Salaam.
Na mimi nikiwa miongoni mwa wanasemina.
Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto.
Katibu Msaidizi wa TASWA George John akifafanua jambo.
Mtoa Mada Salim Said Salim ambaye pia ni Media Consultant (DW/RFI) hapa akitupiga msasa wa kiutuuzima.mhariri wa gazeti la MwanaSpoti Frank Sanga naye alisisitiza wandishi wa habari wa michezo kutobweteka na kuandika habari za wadau na Shirikisho la Soka nchini (TFF) na Vyama mbalimbali vya Michezo kwani zinachosha na kuwataka wanahabari waumize vichwa zaidi pia waandike habari ambazo zenye mtiririko mzuri utakaomvutia msomaji.
0 Comments