Maonyesho na semina ya siku2 ya TWENDE yamalizika Diamond Jubilee.

Hizi ni shanga ambazo huokotwa na katika pwani ya Zanzibar kati ya visiwa vya Tumbatu na ambazo zinaaminika kwamba zilikuwa zikisafirishwa na wafanyabiashara kutoka India na kusafirishwa kote ulimwnenguni kabla ya kuzaliwa Nabii Issa na kwa wakati huo watu walikuwa wakifanya biashara ya kubadilishana bidhaa kwa bidhaa. Shanga hizi hazilingani pia rangi zake ziko tofauti na kadhalika utamaduni wa kuvaa shanga uko duniani kote hivyo muokotaji wa shanga hizi anasema kwamba mtu akiokota shanga kubwa inathamani zaidi ya jiwe la dhahabu hivyo shanga hizi ni za ajabu. Binafsi napenda urembo huu lakini shanga za namna hii sijawahi kuziona na bei yake siyo ya kitoto lazima uvute pumzi.
Pia kuna kitabu kikubwa ambacho kinaelezea umuhimu wa kuvaa shanga, ubora na kila kila kitu kuhusu pambo hilo.

Hapa Muuzaji wa shanga hizo au unaweza kumwita 'Bead Jewellery aliyejitambulisha kwa jina la Teresia Mistry akitoa maelezo mafupi na kusema kwamba hii ni mara yake ya kwanza kushiriki katika semina ya wajasiriamali pia ametoa shukrani kwa mdhamini wake kutoka Zanzibar anakoishi na kufanya biashara hiyo huku akitegemea kuwauzia watalii anaofika Zanzibar.
Teresia akifurahi huku akiwamevaa moja ya shanga azazoziuza.
Hii ni mikufu ya shanga hizo za ajabu hapa zikiwa sokoni.
Nilizishika kuthibitisha ni kweli hazilingani, hapa nikaambiwa zimechanganyika mawe na mchanga wa baharino yote ni mapambo.
Moja ya kurasa zinazopatikana katika kitabu hicho cha masuala ya shanga.
Hata wafale nao walivaa shanga,lakini sikuhizi mmmh wamebaki wanaume wa kabila la kimasai tu.
Haya ndiyo mawe makubwa yanayookotwa ufukweni ambayo yanathamani zaidi ya dhahabu.
Pichani ni moja ya kurasa ikionyesha mfalme na malikia wakiwa wamejipamba kwa shanga.Shanga ya kuvaa shingoni hii ni ya enzi hizo.

TRADE BEAD JEWELLERY BY TERESIA.
originating from Mainland Tanzania,Teresia come to Zanzibar looking for business oppoturnities in the growing tourism industry .she eventually found her nice designing jewellery using materials with a very special history specific in Zanzibar .each year ,during the rainy season ,beutiful coloured beads are washed up on shores of tumbatu Iland north of Unguja .collected by local women for sale ,they said to be remnants of a ship wreck from over 350 years ago.These beads ,commonly called "trade beads",were widely used for commarce by the Arabs during their for reign over the island .Trade beads come in variety of different sizes from the years of saltwater erosion and appear to be made from an assortment of different materials including glass and stone .As each bead is unique in appearance ,all of Teresia's designs are completely individual .Teresia belives made in Zanzibar offers consumers something special "made in Zanzibar is good way to distinguish between quality products mmade on the Island ,those made on mainland Tanzania or Kenya.my beads are from the waters from Zanzibra ,Coconunts products are distincitively Zanzibar .just like the Zanzibars doors ,all of these products are special to Zanzibar .with so much coming from Asia now ,this is very important. Pichani ni baadhi ya vitu mbalimbali vilivyoonyeshwa na wajasiriamali katika semina hiyo.

Post a Comment

0 Comments