Pichani ni Alhaj Muhidin Ndolanga akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani akithibitisha kufanyiwa fujo na wapambe wa waliokuwa wagombea ambao walichakachuliwa kutokana na kutokidhi vigezo vya kuwania nyadhifa za uongozi katika uchaguzi wa Chama Cha Soka Wilaya ya Temeke (TEFA).
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Alhaji Muhidin Ndolanga, mchana wa leo amenusurika kupigwa na wapambe wa wagombea watatu walioenguliwa katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Soka Wilaya ya Temeke (TEFA) utakaorindima Septemba 19 katika ukumbi wa JKT Mhulani Jijini Dar es Salaam.Ndolanga amekiri kwa kusema kuwa wapambe wagombea hao walivamia Ofisi za (DRFA) majira ya saa sita mchana na kumfanyia fujo huku wakimtaka Ndolanga kuwarudisha katika kinyang’anyiro cha uchaguzi huo wagombea walioenguliwa kwa madai kuwa Kamati ya Uchaguzi ya (TEFA) haikuwatendea haki kwa kuwaengua na kwamba wana vigezo vya kushiriki katika uchaguzi huo.Ndolanga aliwataja walioenguliwa kuwa ni Abdulhabib Abdallah, aliyekuwa anawania nafasi ya Mwenyekiti, Azizi Mohamed, Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti na Omari Abdulkadir, aliyekuwa anawania nafasi ya Ujumbe wa Mkoa.Aidha Ndolanga, alisema uaamuzi ya Kamati ya Uchaguzi wa kuwaengua wagombea hao utabakia pale pale na kusisitiza kufanyika kwa uchaguzi huo kama ilivyokwisha kupangwa.Ndolanga, mwenyekiti aliwahi kuwa Mwenyekiti Chama cha Soka Tanzania (FAT) alisema tayari tukio hilo limesharipotiwa Kituo cha Polisi Msimbazi na kupewa RB; MS/RB10208/2010 kwa ajili ya Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa vurugu hizo.Wagombea wanaochuana katika kinyang’anyiro hicho kwa upande wa mwenyekiti ni Peter Mhinzi na Msanifu Kondo, Makamu wa kwanza wa mwenyekiti ni Meba Ramadhani na Saleh Mohamed huku Makamu wa pili wa Mwenyekiti akiwa Bakili Makere, Juma Lunje na Siza Chenja.Kwa upande wa ujumbe wa kuwakilisha mkoa ni Francis Peter, mweka hazina Abraham Barabara na Yusuf Kinega wakati mweka hazina msaidizi ni Heri Kaiza.Wajumbe ni Albino Lwira, Fikiri Magoso, Hamis Balawa, Obby Steleki, Ally Kulita na Mfaume Ramadhani.
0 Comments