SERIKALI ya Tanzania inatarajia kuingia mkataba wa maendeleo ya michezo na Taasisi ya michezo kwa wote (TAFISA) yenye maskani yake Ujerumani.Akizungumza na waandishi wa habari jana Katibu Mkuu wa TAFISA, Wolfgang Baumann alisema mkataba huo Tanzania itaingia na Chuo cha Maendeleo ya Michezo cha Malya cha jijini Mwanza.Baumann alisema juzi na jana walizuru chuoni Malya kwa ajili ya kujionea mazingira ya rasilimali zilizopo chuoni hapo ambazo walikubali kushirikiana na Tanzania katika maendeleo ya michezo. Naye mweka hazina wa TAFISA, Brian Dixon alisema Baumann anatarajia kurejea Tanzania Novemba kwa ajili ya kumalizia mazungumzo na serikali ya Tainzania. Dixon alisema sababu za kuunganisha nguvu na Tanzania ni kutokana na sababu kwamba mojawapo ya viongozi wa TAFISA ni Mkurugenzi wa Michezo wa Tanzania, Leonard Thadeo ambaye ni Makamu wa rais wa TAFISA.
DKT. NCHEMBA AMUAGA BALOZI WA MAREKANI NCHINI
-
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema kuwa
Tanzania ina thamini mchango mkubwa wa Taifa la Marekani ka...
6 hours ago
0 Comments