TBL wasaini mkataba wa miaka 3 na Bongo Star Search.

Memeja wa Kinywaji cha Bia ya Kilimanjaro George Kavishe akizungumza na wanahabari hawapo pichani.

KAMPUNI ya Bia Tanzania kwa kupitia kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager wametoa udhamini wa sh. millioni 100 kwa shindano la Bongo Star Search ambazo zitatumika kwa mwaka huu, pia wadhamini hao watadhamini shindano hilo kwa miaka 3 mfululizo.Akizungumza jana katika mkutano na waandishi wa habari , Meneja Udhamini wa Bia ya Kilimanjaro Emmanuel Kavishe alisema.Bongo Star Search ni moja ya kipindi kinachorushwa hapa nchini ambacho kimefanikiwa kwa kiwango kikubwa kabisa kuinua vipaji vya wanamuziki wa Kitanzania.
Ikumbukwe mwaka jana Kampuni ya TBL kwa kupitia kinywaji chake kinachojihusisha na maswala ya muziki Kilimanjaro Premium Lager, ilishiriki kama mmoja wa wadhamini shindano hili.
“Uhusiano huu mkubwa wa Kampuni hizi mbili umetokana na sababu kuu kwamba BSS inahusika kutafuta na kuinua vipaji vya wanamuziki hasa vijana wenye umri wowote ambapo Kilimanjaro Premium Lager , kufuatia kauli mbiu yake ya kufikisha muziki wa Tanzania katika kilele cha mafanikio kwa upande mwingine ina husika na muziki wa vijana wa hapa nchini” alisema Kavishe.
Aidha kinywaji cha Kilimanjaro kimekuwa kikiunga mkono juhudi za kuendeleza muziki hapa nchini kwa kiwango cha juu ambapo mara kadhaa wamekuwa wadhamini wa utoaji Tunzo za Muziki Tanzania (TMA), ndiyo maana TBL imeona hakuna sababu ya wao kutoshirikiana na BSS 2010 katika kuinua vipaji vya wanamuziki nchini kwa ujumla.
Kavishe ameendelea kwa kusema kuwa TBL tayari imesaini mkataba wa kudhamini Bongo Star Search kwa kipindi cha miaka mitatu ambayo ni kati ya 2010 hadi 2012.Washiriki wa shindano hilo watapata fursa ya kushirki katika mambo mbalimbali yakiwemo mashindano yatakayokua yanafanyika katika jumba la BSS Kili House 2010.
BSS 2010 itakua ikirushwa hewani kila siku ya Jumapili kuanzia saa 3:15 kwa kupitia kituo cha Runinga cha ITV sanjari na Redio One, mashabiki watatakiwa kuwapigia kura .
Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Production ambao ndiyo waratibu wa shindano la BSS , Rita Paulsen akizungumza mbele ya waandishi wa habari ambako aliweka wazi kuwa amefurahi sana kutokana na udhamini wa miaka 3 aliopata kutoka TBL yaani utakuwa wa 2010 hadi 2011.Ameahidi kuboresha zawadi kwa mshindi wa mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments