KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Jan Poulsen jana alitaja majina ya wachezaji 7 ambao wameachwa katika kikosi cha nyota 26 kwa ajili ya kampeni ya kusaka tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2012 nchini Benin na Equatorial Guinea ambapo Stars itaanza na Algeria.Poilsen alisema kwamba wataondoka na wachezaji 20 huku walioachwa ni Uhuru Suleiman, Juma Jabu, Jerson Tegete, Juma Kaseja, Abdulhalimu Humoud, Kevin Yondani na Athuman Idd ‘Chuji’.Alisema timu yake imejiandaa vyema na michuano hiyo kwa kuwa hadi sasa hakuna majeruhi , na kuongeza kuwa Juma Kaseja ataendelea kukaa benchi kwa wiki moja zaidi hivyo hakukuwa na sababu ya kumpanga.
Wengine watakaowakilisha ni makipa Shaban Hassan (Mtibwa Sugar), Jackson Chove (Azam FC ) Mabeki: Shadrack Nsajigwa (Yanga), Salum Kanoni (Simba), Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Stephano Mwasika (Yanga) ,Viungo walioitwa katika kikosi hicho cha Poulsen aliyeanza kazi hiyo Agosti mosi akichukua nafasi ya Mbrazil, Marcio Maximo, ni Henry Joseph (Kongsivinger IL Norway), Jabir Aziz (Azam), na Nurdin Bakari (Yanga).Wengine ni a),Seleman Kassim (Azam) na Idrisa Rajabu (Sofapaka-Kenya).
Akitangaza majina hayo jana katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) ,washambuliaji ni Danny Mrwanda (DT-Long AN-Vetinam), Nizar Khalifani (Vancover White Caps-Canada/USA), Mrisho Ngassa (Azam, Mussa Hassan ‘Mgosi’ na John Bocco (Azam) .Uteuzi huo umekuja baada ya wachezaji hao kufanya mazoezi kwa wiki kadhaa, hivyo amewachuja na kubaki 20 kwa ajili ya kuwakabili Algeria hapo Sepemba 3, itakayochezwa mjini Algiers ambapo Stars itaondoka Agosti 31 kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Qatar .
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA UKIMWI YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA AFUA
ZA UKIMWI NJOMBE
-
NA. MWANDISHI WETU – LUDEWA
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI,
Mheshimiwa Dkt. Elibariki Kingu ametoa piongezi kwa M...
7 hours ago
0 Comments