Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habri za Michezo (TASWA), Juma Pinto akizungumza na wanachama kwa mara ya kwanza kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Karume Dar es Salaam.Pinto ametangaza kuwa TASWA kama chama kimewasiliana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa kupitia barua kueleza adhama yake ya kumtunukia Tunzo maalum na ya heshima kwa mchango wake katika kunedeleza michezo nchini .Mfano ujio wa aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' Mbrazil Marcio Maximo na kulipwa mshahara na serikali, ujio wa Kocha wa ngumi na hivi karivunikocha wa riadha.Kwa kutumia nafasi hiyo ya kukutana na Rais uongozi wa TASWA utawasilisha maombi na mapendekezo mbalimbali kuhusiana na maendeleo ya chama na waandishi wa michezo nchini kwa ujumla.Aidha TASWA mpya imeng'oa utaratibu wa kumpata mwanamichezo bora kwa kila mwezi hivyo atasakwa mara moja tu ambapo kuanzia mwakani atatafutwa mwanamichezo bora wa mwaka huku jukumu hilo lilipelekwa kwa uongozi wa vyama, mtangazaji bora, mwandishi bora wa habari jukumu la kuwachagua washindi likipelekwa kwa wahaririri katika kila chombo ambao watapendekeza majina,hafla hiyo imepangwa kufanyika Februari mwakani.
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA AFYA NA UKIMWI YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA AFUA
ZA UKIMWI NJOMBE
-
NA. MWANDISHI WETU – LUDEWA
MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI,
Mheshimiwa Dkt. Elibariki Kingu ametoa piongezi kwa M...
4 hours ago
0 Comments