UDSM YAJIPANGA KUBADILI MITAALA KUENDANA NA SOKO LA DUNIA


Mkuu wa Shule ya Biashara nchini Qatar Prof. Habib Mahama raia wa Ghana yupo nchini akitoa mafunzo ya siku mbili kwa Wahadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM).

Dkt. Theresia Dominic wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam amesema katika mafunzo yao ya siku mbili yanayoongozwa na Mtaalam wa Miradi kutoka Chuo Kikuu Cha Qatar Prof. Mahama atawafundisha namna ya kuboresha mitaala yao ili wasomi kutoka nchini waweze kuajiriwa Kimataifa.

Amesema hayo katika mafunzo ya siku mbili yanayoendelea Shule ya Uongozi Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani.

"Mtaalamu huyo kutoka Chuo Kikuu Cha Qatar atatufundisha namna ya kuboresha mitaala yetu na mabadiliko ya mitaala inatakiwa ianzie ngazi ya chuo kikuu kwenda ngazi zingine za chini za elimu" amesema.

"Faida ya maboresho hayo ya mitaala ni kwamba wale watakao pata elimu katika Chuo Kikuu hicho wataweza kuajiriwa katika taifa lolote duniani kwasababu mitaala itakuwa inalingana na Vyuo vingine dunianii".
Mratibu wa Mradi huo Dkt. Mesia Ilomo Mhadhiri Mwandamizi kutoka UDSM Idara ya Elimu na Fedha 
amesema kuwa 
Mradi huu unalenga kujengea uwezo kwenye Shule Kuu za Biashara Afrika
yanaangalia masuala ya utaalam ,masoko,mipango mikakati na Vyuo kutoa wahitimu bora kwa kuzingatia soko Kimataifa
Prof Habib  Mahama  ambaye ni Mkuu wa Shuke ya Biashara Qatar  .
Prof. Omar Mbura Mkuu wa Shule Kuu ya Biashara Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) amesema mafunzo hayo yataangazia jinsi Chuo Kikuu Cha Biashara Qatar ambacho ni Chuo bora kati ya vyuo 250 duniani kujifunza mbinu za kubadili mitaala itakayoendana na wakati na kuwa na mipango mirefu itakayoleta tija kwa wasomi nchini.

"Mabadiliko hayo ya mitaala yatawezesha chuo kikuu hicho kuwa miongoni mwa vyuo vikuu bora duniani "amesema  Prof. Mbura.


 

Post a Comment

0 Comments