Ikiwa ni katika kusherehekea miaka 65 ya kuzaliwa Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu
Hassan inayoadhimishwa kesho tarehe 27 Januari 2026, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge kesho ataongoza zoezi la kupanda miti sambamba na kugawa miche 1500 ya mikorosho itakayogaiwa Wilayani Rufiji.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo tarehe 26 Januari 2026,RC Kunenge amesema "Kwa niaba ya serikali ninayofuraha kuwaambia wananchi wa Mkoa wa Pwani kesho ni siku ya kuunga mkono juhudi na maono yake ya kulinda na kutunza mazingira,Mkoa wa Pwani utaendesha zoezi la kupanda miti 6,379 ambapo miti ya mbao na vivuli.
Idadi hii ni sehemu ya miti 13,500,000 itakayopandwa na Halmashauri zote wakati wa mvua za masika.
Miti 6,379 itapandwa kwenye maeneo ya Shule ambako wanafunzi wataihudumia.
Zoezi hili litakwenda sambamba na uzinduzi wa upandani miti Mi.1,500,000 ya Mikorosho itagawiwa kwa wakulima wa Rufiji.
Kauli mbiu yetu inasema uzalendo ni kutunza mazingira shirikishi kupanda miti.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Kunenge ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Pwani kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo la upandaji na ustawi wa jamii.

0 Comments