Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Alhaj Abubakar Kunenge, ameongoza wakazi wa Chumbi A, Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani, katika zoezi la upandaji miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu HHassa leo tarehe 27 Januari 2026.
Zoezi la upandaji miti limefanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Chumbi A, wilayani Rufiji, ikiwa ni sehemu ya shughuli za kumbukizi hizo.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, jumla ya miti 6,379 imepandwa katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Pwani, ikijumuisha miche ya vivuli, matunda na miti ya mbao.
Viongozi wengine walioshiriki katika zoezi hilo ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Luteni Kanali Faustine Komba, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rufiji, Mussa Hemed, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Simon Berege, pamoja na madiwani na wananchi wa eneo hilo.Wakati huohuo, Mkoa wa Pwani umegawa miche ya mikorosho milioni 1.5 kwa wakulima wa Chumbi A, Wilaya ya Rufiji, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha kilimo na uhifadhi wa mazingira.






0 Comments