ULINZI WAIMARISHWA MKUTANO WA WAKUU SADC NA EAC


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kufuatia Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambapo Mkutano chini ya uenyeji wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hali ya usalama imeimarishwa mara dufu February 07, hadi 08, 2025 na baadhi ya barabara zitakuwa zinafungwa kwa muda na kufunguliwa haraka kupisha misafara ya Viongozi wa mkutano huo. 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema barabara ambazo zitafungwa kwa muda na kufunguliwa haraka kadri itakavyoruhusu ni barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji, barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu.

Nyingine ni barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena, barabara ya Garden kutokea barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya
Southern Sun “Katika kipindi chote cha mkutano huo, Watumiaji wengine wa barabara mnashauriwa kutumia barabara za Uhuru, Kawawa kupitia Magomeni, Kigogo kuelekea Temeke, barabara ya Morogoro na Msimbazi, Morogoro na
Lumumba na kwa wale wanaotokea maeneo ya Chanika wanashauriwa kutumia njia mbadala ya mradi ya SGR ili waje kutokea barabara ya Mandela na Uhuru”

“Jeshi litajitahidi kupunguza usumbufu kwa kufanya kazi ya ziada kwenye barabara hizo kwa kuzifunga na kuzifungua haraka kadri msafara utakavyokuwa unapita, kwasababu za kiusalama wale wanaotumia vyombo vya moto kama pikipiki za magurudumu mawili (bodaboda) na magurudumu matatu (bajaji)
vyombo hivyo vitazuiwa kwa muda maeneo hayo yaliyotajwa kwa sababu za kiusalama wakati wa ugeni huu ukipita kwenye njia watakazokuwa wakipita”

Post a Comment

0 Comments