DC MAGOTI KUONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA JENGO LA VIP KISARAWE

 DC wa Kisarawe Petro Magoti  akipokea kitenge ambacho ndiyo sare itakayovaliwa siku ya hafla ya Kisarawe Afya Gala itakayofanyika tarehe 2 Novemba 2024,akimkabidhi  mjumbe wa Kamati Kisarawe Afya Gala Asia Mohammed. 

Mkuu wa Wilaya  Magoti ametoa wito kwa Viongozi ,wafanyabiashara wakulima na  wadau mbalimbali wanaoishi   ndani na nje ya nchi kujitokeza katika uchangishaji wa fedha za ujenzi wa jengo la VIP na ukarabati wa majengo ya  Hospitali ya Kisarawe  ambayo yamechakaa kwa sasa.

Mhe.Magoti amesema hayo jana  18,Oktoba alipozungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika  ofisini kwake.

DC Magoti amesema kuwa hafla hiyo inafahamika kama Kisarawe Afya Gala imepangwa kufanyika tarehe 2 Novemba 2024 ambapo  uchangishaji fedha utafanyika   kwenye Ukumbi wa Minaki Sekondari  uliopo  Kisarawe.

"Nachukua fursa hii kuwakaribisha  wadau wote  katika  Kisarawe Afya Gala ikiwa na lengo la kufanya harambee ya  kuchangia  fedha zitakazofanya  ukarabati wa majengo yaliyochakaa na ujenzi wa jengo la VIP la kisasa labisa amesema "DC Magoti.

Aidha DC Magoti amesema kuwa mgeni rasmi  katika hafla hiyo ya Kisarawe Afya Gala atakuwa Waziri wa Viwanda na Biashara  Dkt.Selemani Jafo  ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo pia wanatarajia kuwa na mgeni maalumu ambaye ni Waziri wa Afya Mhe.Jenista Mhagama.

Wakati huohuo DC Magoti katika kuchagiza  Kisarawe Afya Gala amenunua kitenge ambacho ndiyo vazi maalumu siku hiyo kwa sh.100,000  na amesisitiza wadau wanunue ikiwa ni nji ya kuchangia hafla hiyo.

DC Magoti  ametaja namba zinazopokea mchango kuwa ni  Tigo 17403829 jina KISARAWE  AFYA GALA na 21410007917 NMB. 

Wakati huohuo  Mganga Mfawidhi  wa Hospitali  ya Kisarawe Yonah Kabata amesema kuwa ujenzi hilo jengo   utagarimu kiasi cha Mil.900 ambapo pia wamepanga jengo hilo la VIP lishabihiane na    majengo  ya Taasisi ya Jakaya Kikwete huku mgonjwa akiwa wodini apate huduma ya kiyoyozi ,
luninga na chakula. 

"Katika Hospitali  yetu tunatibu wagonjwa wengi hasa ikizingatiwa tuko karibu na mbuga ya Seluu watalii wanaokwenda huko pindi wakipata changamoto  za afya wanaletwa hapa  na wakiletwa wengi hushangaa hali ya uchakavu wa majengo yetu japo wengi wao huwa wako tayari kulipia gharama  kiwango chochote cha fedha  jambo ambalo limetupa msukumo  wa kujenga jengo hilo la VIP la kisasa na kufanya ukarabati kwa majengo  yote chakavu hospitalini hapa
DC Petro Magoti akimkabidhi kiasi cha Sh.100,000 ambayo ni malipo ya sare ya Kisarawe Afya Gala  mwakilishi wa waratibu wa hafla hiyo  itakayofanyika tarehe 2Novemba ,2024 anayepewa fedha hizo ni Mjunbe wa Kamati ya Kisarawe Afya Gala Bi Asia Mohammed. 

Post a Comment

0 Comments